Hapa wanasalimiana katia ya mku wa mkoa wa katavi na mkurugenzi wa GBP TZ
Mkurugenzi wa GBP Tanzania Rashid Seif Soud akimwelekeza mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga sehemu ya kukata utepe wake
RC katavi akizindua kito kipya cha mafuta cha kampuni ya GBP Mpanda
Na Walter Mguluchuma .
Katavi.
Wawekezaji
katika sekta ya mafuta mkoani katavi wameiomba serikali kulipatia
ufunbuzi changamoto ya miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha
usafirishaji wa mafuta kutoka Dares salam hadi mkoani Katavi kufutia
kujitokeza kwa wawekezaji wa mafuta kujenga vituo vya mafuta ambapo
kampuni ya GBP imejenga kituo cha mafuta chenye thamani ya zaidiya
milioni 500 Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na kupunguza adhaa ya
upatikanaji wa mafuta katika mkoa huo wenye mahitaji kwa sasa kutokana
na kuwa bado mkoa mchanga,
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha mafuta kinachomilikiwa na
kampuni ya GBP ambaye ni mwekezaji kwenye sekta ya mafuta hapa nchini
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Rashidi Seif Soud ameleza kuwa chanagmoto ya
miundo mbiu ya barabara katika mkoa huo bado ni changamoto kubwa,
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa pamoja na kuwepo changamoto wao
kama wazao wa mkoa wa katavi wataendelea kuwekeza katika mkoa huo kwa
kuwa kampuni ya GBP chimbuko lake ni Mpanda Mkoa ni Katavi.
Amefafanua
kuwa kampuni hiyo ambayo inamatawi yake karibu mikoa yote nchi ikiwa
imejikitazaidi katika mikoa ya kanda ya ziwa na ukanda wa magharibi
mikoa ya Mwanza ,Simiyu Geita,Kagera,Mara na Shinyanga,Vilevile inayo
matawi Zanzibar,Dar,Arusha na Mbeya pia matawi mengine yako katika
mikoa ya Kigoma Tabora na Katavi pamoja na nchi ya jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo DRC.
Aidha
ameleza kuwa katika kutekeleza azma ya serikali ya awam ya tano ya Dkt
Pombe Magufuli ya Tanzania ya Viwanda na kuzalisha ajira wao kama
wawekezaji wameweza kuzalisha ajira zaidi ya 1000 hapa nchini na ni moja
ya Kampuni ya Mafuta inayoongoza katika ulipaji wa kodi ambapo kwa
miaka miwili mfulizo wamekuwa wakilipa kodi bila matatizo
Katika
uzinduzi huo Mkurugenzi huyo ametoa mifuko 500 ya saruji kwa mkuu wa
mkoa wa Katavi itakayosaidia katika ujenzi wa kiwanja cha michezo
kilichoanza kujengwa Mwaka huu, na kilitumika katika uzinduzi wa mbio za
mwenge kitaifa wakati wa uwashaji wake uliofanyika mwezi April 2 mwaka 2017.na sasa unaendelea kujengwa taratibu kwa ajili ya shughuli nyingine za michezo.
Hivyo
kufunguliwa kwa kituo hicho kitasaidia kwa njia moja au nyingine
kuwahuduamia wananchi na kitaongeza ajira kwa wananchi walio wengi hapa
mkoani.
Akiongea
katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael
Muhuga amepongeza juhudi zilizochukuliwa na wawekezaji hao kuwekeza
katika mkoa wa katavi,na kueleza kuwa hata wengine waige mfano huo
kuliko kwa kuwa wapo wanakatavi wengi walioko nje ya mkoa wa katavi na
uwezo wanao lakini hawataki kuja kuwekeza wanataka waletwe wakiwa
wameisha kufa niyo waletweMpanda inakuwa haiana maana ni vyema wakaja
kuwekeza wakiwa bado wako hai.
Akizungumzia
miundo mbinu ya barabara amaesema serikali inaendelea kuhakikisha
inatengeneza miundombinu hiyo ya barabara kwa kuwanza ujenzi wa lami
katika baabara ya Mpanda Inyonga hadi Tabora inayoanza kujengwa mwezi
ujao .
Pia
serikali inaendelea kuhakkiisha inaboresha miundo mbinu ya barabara kwa
kujenga kwa kiwango cha lami ambao barabara ya kutoka Mpanda Stalike
kwa kiwango cha lami imekamilika na Sasa inaendelea kujengwa ya kutoka
Mpanda kilometa 30 kuelekea mkoani kigoma wakati wakandarasi wengine
wameanzia uvinza mkoani Kigoma kuelekea mpanda,juhudi
zinaendeleakuhakikisha uimarishaji wa miundo mbinu hiyo inaimarika ili
kukabiliana na changamoto hiyo hivyo wawekezaji wasiogope kuja kuwekeza
katavi.
Akizungumzia ujenzi wa
uwanja wa michezo amepongeza na kushukuru kwa msaada uliotolewa na
Mkurugenzi wa GBP kutoa mifuko 500 ya saruji itakayosaidia katika ujenzi
wa uwanja huo, akahimiza na wengine wajitokeze kuchangia chochote ili
kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.
Pia
akashukuru kwa njia moja au nyingie=ne wale waote waliojitolea kwa hali
na mali katika ujenziwa uwanja huokuanzia wananchi wajasiliamali
wafanyabiashara na makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali zikiwemo
Halmashauri za wilaya zilizoko mkoani hapa.
Wily
Mbogo ni Meya wa Halmashauri ya Mpanda ameshukuru kwa uwekezaji mzuri
kwa kuwekeza fursa nzuri ya kukuza uchumi pamoja na misaada ya mifuko
500 ya saruji na kisima kirefu cha maji kwa ajili ya wananchi wa Kata ya
Majengo Halmashauri ya Mpanda.
Nasoro
Alfi ni Mwenyekiti wa Usafirishaji mkoa wa katavi amehimiza watumiaji
wa vyombo vya moto kutumia kituo hicho kwa kuwa kitasaidia kwa njia moja
au nyingine kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mafuta unaokuwa
unajitokeza mara kwa mara katika mkoa huo wa Katavi,na watoe
ushirikianao wa karibu.
Nao
wananchi katika Mkoa wa Katavi Fatuma Rashi na wamepongeza moyo
ulioneshwa na mwekezaji na kueleza kuwa kuwepo kwa uwekezaji huo
kutasaidia kuongeza ajira kwa vijana na huduma nzuri kwa watumiaji wa
vyombo vya moto hivyo wamuunge mkoano na kumpatia ushirikiano mkubwa
mwekezaji huyo.
0 comments:
Post a Comment