Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Shirika la Marie Stopes Tanzania ilimetowa elimu kwa Wanafunzi wa Shule kumi za Sekondari za Manispaa ya Mpanda ya juu ya uzazi wa mpango na afya ya msingi na namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU.
Shirika hilo lilitowa elimu hiyo wakati wa kongamano la situ tatu ambapo maadhimisho yake yalifanyika jana katika uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili katika Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa .
Mratibu wa Vijana Marie Stopes Tanzania Daniel Mjema Emanuel alieleza kuwa kongamano hilo liliandaliwa na shirika la Marie Stopes Tanznia kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Alieleza kuwa lengo la kongamano hilo la siku tatu ilikuwa ni kutowa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari na kwa vijana ambao sio wanafunzi yenye lengo la kuwapati Afya ya msingi,uzazi wa mpango na namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU pamoja na kujiepusha na mimba za utotoni .
Alisema katika kongamano hilo wametowa furusa pia ya watu kujipima na kutambua afya zao na wameweza kutowa pia elimu ya afya ya uzazi kwa watu mbalimbali waliofika kwenye kongamano hilo.
Nae mratibu wa Marie Stopes Mkoa wa Katavi Seif Kijiko alieleza kuwa Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo inaongezeko kubwa la mimba za utotoni kwa wasichana wenye umri mdogo .
Alifafanua kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo la mimba za utotoni Marie Stopes wamekuwa wakitowa elimu mbali mbali kwenye mashule ya sekondari na katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu katika maeneo yote ya Mkoa wa Katavi .
Kijiko alisema licha ya jitihada hizo zinazofanywa na shirika hilo wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali na alitaja baadhi ya changamoto iliyopo kuwa nia.
Baadhi ya walimu wa shule za Sekondari wamekuwa wakikataa kutowa ushirikiano kwa Marie Stopes kwa kukataa elimu ya afya na uzazi wa mpango isitolewe kwenye shule zao .
Kwa upande wake Mraribu wa afya na uzazi wa mpango wa Manispaa ya Mpanda Muna Sumry alieleza kuwa Manispaa ya Mpanda wameanza kutowa elimu kwenye shule za msingi juu ya madhara ya kupata mimba za utotoni ikiwa ni hatua moja wapo ya kupunguza tatizo la mimba za utotoni .
Mgeni rasmi wa kongamano hilo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Willbard Marandu alieleeza kuwa tatizo la wasichana kubeba mimba wakiwa na umri mdogo umekuwa ukisababisha vifo vya mama na mtoto .
Alisema imani potofu imekuwa ikichangia watu kutofuata uzazi wa mpango kwani wanaamini kuwa mwanamke ni chombo cha kuzaa watoto hivyo hari hiyo imekuwa isababbisha watu kuzaa ovyo ovyo bila kufuata uzazi wa mpango na kuwa na familia kubwa ambayo hushindwa kuitunza.
Velinaice Godwin Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda eleleza kuwa elimu walipatiwa na Marie Stopes imewasaidia sana kutambua umuhimi wa uzazi wa mpango na jinsi ya kujiepusha na mimba za utotoni na kujikinga na maambukizi ya VVU.
0 comments:
Post a Comment