Mpanda
KAYA zaidi ya 80 kutoka kitongoji cha Kitupa wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi hawana makazi ya kudumua na kulazimika kulala nje usiku baada ya nyumba zao kubomolewa ili kupisha upanuzi wa eneo la mnada .
Baadhi yao wameleza kuwa nyumba zao zilibomolewa juzi saa sita mchana na askari wa Hifadhi za Taifa (Tanapa) wakishirikiana na askari wa jeshi la akiba maarufu mgambo ambapo sasa wanalazimika kulala nje na wake zao karibu na watoto na wakwe zao ikiwa ni kinyumbe na mila na dessturi zao .
Mkazi wa kitongoji hicho , Eliasa Chimbamawe alidai kuwa wazazi wake walijenga na kuishi hapo tangu mwaka 1949 hadi walipoaga dunia mwaka 1975 na kuzikwa hapo .
Nae Festo Lazaro alieleza kuwa yeye na familia yake walilazimishwa kubomoa nyumba yao na askari hao huku akiamriwa kuimba nyimbo za hamasa ili wasichoke .
Kwa upande wake Anoneta Joseph ambaye ni mjane alidai kuwa nusura watoto wake watatu wapoteze maisha ambapo walizimia baada ya kuelezwa na wenzao kuwa nyumba yao imebomolewa na askari .
Meda Shigela aliyedai kuwa ana watoto 13 alijenga na kuanza kuishi hapo tanguj 1997 ambapo sasa amelazimika kulala nje usiku na mke wake , watoto na wakwe zake ikiwa ni kinyume na desturi na mila zao .
Mpelwa \John alidai kuwa mbaya zaidi licha ya nyumba zao kubomolewa pia vyoo vimetekelezwa na sasa wanalazimika kujisaidia porini huku wakihofia kulipuka kwa magonjwa ya kuhara ikiwemno kipindupindu.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Kitupa Mkamba Mzoloka alidai kuwa wakazi wake wanateseka kwa kukosa makazi ya kudumu ambapo walibomolewa nyumba zao bila kutaarifiwa kwanza .
0 comments:
Post a Comment