Na Walter Mguluchuma .
Askaari Polisi Konsitebo Peter Kashuta wa kituo cha Polisi Mwese Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh laki tano baada ya kuapatikana na hatia ya kuomba na kupokea Rushwa ya SHS 700,000 .
Mshitakiwa huyo alihukumiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahamani hapo na upande wa mashitaka uliongozwa na wanasheria wa TAKUKURU Bahati Haule na Simon Buchwa .
Hakimu Ntengwa kabla ya kusoma hukumu hiyo alisema kutokana na ushahidi uliotplewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi wanane na mshitakiwa hakuwa na shahidi hata mmoja Mahakama iliridhika na ushahidi wa vielelezo vilivyotolewa Mahakamani hapo fedha za mtego na jelada la kesi aliokuwa akiichunguza mshitakiwa kama ushahidi katika kesi hiyo.
Alisema pamoja na mshitakiwa Peter Kashuta kujitetea kuwa wakati anakamatwa na maafisa wa TAKUKURU yeye hakuna na pesa yoyote ili aliyokutwa nayo .
Chiganga aliendelea kusoma hukumu na kueleza kuwa Mahakama imeona kuwa kitendo cha mshitakiwa kukimbia na kisha kuanza kupigana na maafisa wa TAKUKURU kwa kipindi kirefu na baada ya kuzidiwa aliamua kuzitupa fedha hizo ilikuwa ni vigumu kuweza kushika nazo fedha zikiwa mfukoni wala mkononi kwani alikuwa ameisha zitupa .
Alisema ushahidi mwingine uliomtia hatiani mshitakiwa atiani ni kitendo cha kufuata mshitakiwa Hotelini ambae alikuwa amepanga nae ili wakabidhiane kiasi hicho cha fedha ili aweze kumsaidia kwenye kesi yake .
Akitowa adhabu hiyo Hakimu Ntengwa alisema Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa kwa kosa la kifungu cha sheria Namba 15 cha sheria ya kupambana na kuzuia rushwa sura ya 11 ya mwaka 2007.
Hivyo kutokana na makosa hayo mawili ya kuomba na kupokea Rushwa kwenda sambamba Mahakama imemsamehe kwa kosa la kuomba Rushwa ila imemuhukumu kwa kosa la kupokea Rushwa hivyo mshitakiwa Peter Kashuta mahakama imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Tshs 500,000.
Awali katika kesi hiyo waendesha mashita wanasheria wa TAKUKURU Bahati Haule na Simon Buchwa walidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Februari 9 mwaka jana huko katika Kijiji cha Mwese Wilaya ya Tanganyika .
Siku hiyo mshitakiwa alidaiwa kuomba Rushwa ya Tshs 700,000 kutoka kwa Luchega Mambalu ambae alikuwa amefunguliwa kesi katika kituo cha polisi Mwese hata hivyo Luchega aliamua kwenda kutowa taarifa Takukuru na ndipo walipoandaa mtego na kufanikiwa kumkamata mshitakiwa Peter siku hiyo.
Hata hivyo mshitakiwa aliweza kuponyoka kwenda kutumikia kifungo jela baada ya kulipa faini ya shilingi laki tano na kuweza kuwa huru.
0 comments:
Post a Comment