Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wavamia Kijiji na kuwapora Wafanyabiashara wa maduka wa Kijiji cha Itenka Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 4 baada ya kuwatishia kwa kulipua milipuko ya baruti na kusababisha wafanya biashara kukimbia na kuacha maduka yao wazi .
Kaimu Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kataji Benedict Mapujila alisema tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa moja na nusu usiku katika eneo la kijiji cha Itenka Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mpanda .
Alisema siku hiyo ya tukio majambazi hao watano walifika kwenye eneo hilo na kuwavamia wafanyabiashara kwa kulipua baruti hewani hari ambayo iliwafanya wafanyabiashara wa maduka wakimbie na kuwacha maduka yao yakiwa wazi .
Kaimu Kamanda Mapujila alieleza kuwa baaada ya wafanya biashara hao kuwa wamekimbia na kuwacha wazi maduka yao majambazi hao hao waliingia ndani ya maduka mawili na kupora kiasi cha Tsh 4,300,000 na kisha walitokomea mahari kusiko julikana .
Wananchi wa Kijiji hicho walitowa taarifa kwa jeshi la Polisi juu ya tukio hilo na polisi walifika katika eneo hilo baada ya muda mfupi na walianza msako wa kuwasaka majambazi hao na hata hivyo hawakufanikiwa kuwakamata .
Alisema polisi walifanya uchunguzi kwenye eneo hilo na hawakuweza kufanikiwa kuokota ganda lolote lile la rissi na kushiria kuwa majambazi hao hawakuwa na risasi bali walitumia baruti kwenye tukio hilo.
Kaimu Kamanda alisema hadi sasa kakuna mtu yoyote ambae amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la polisi linaende na msako mkali ili kuweza kuwakamata watu waliohusika kwenye tukio hilo la uporaji .
Alieleza kuwa jeshi la polisi limeimrisha ulinzi kwenye kipindi hiki cha sikuuu na ndio maana polisi waliweza kufika kwenye eneo hilo muda mfupi tuu mara baada ya kutokea kwa tukio na amewaomba wananchi kutowa ushirikiano kwa jeshi la polisi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment