Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wakazi wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wanatarajia kupata umeme wa orio utakao wafanya waondokane na tatizo la kukatikatika kwa umeme na baadhi ya vijiji katika Wilaya ya Tanganyika vitanufaika na mradi huo vijiji ambavyo wananchi wake hawaja wahi kuona umeme wa nguzo ya umeme toka Wilaya hiyo ilipoanzishwa .
Msimamizi wa mradi huo Eng Stephen Manda aliwaambia jana Madiwani wa Maspaa ya Mpanda waliotembea mradi huo wa mashine za kusambaza umeme kuwa mradi huo umegharamiwa na Serikali ya Uholanzi kwa kushilikiana na Serikali ya Tanzania na utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 20.5.
Alisema mradi huo wa umeme wa Orio upo katika hatua za mwisho na utakamilika mwezi watano mwaka huu ambapo ulipangwa kuwa umekamilika mwezi julai mwaka huu ukiwa umekamilika miezi miwili kabla ya muda uliokuwa umepangwa na kwa hapa nchini ni mradi watatu miradi mingine kama huo imefanyika atika wilaya za Ngala na Bihalamlo Mkani Kagera.
Mradi huo katika Wilaya ya Mpanda utafika umbali wa kilometa 79 na kuweza kufika hadi katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Tanganyika ambavyo wananchi wake hawaja wahi kuuwona umeme wala nguzo za umeme toka Wilaya hiyo ilipoanzishwa wakati wa Mkoloni mwaka 1949 wakati huo I wakiwa katika Wilaya ya Mpanda kabla ya kuanzishwa mwaka jana Wilaya ya Tanganyika .
Alifafanua kuwa vijiji ambavyo vitanufaika na umeme huo katika Wilaya ya Tanganyika ambavyo havija wahi kuona nguzo za umeme ni Kabungu ,Mchakamchaka ,Ifukutwa , Sijonga na pia umeme uwo utafika katika Gereza la kilimo la Kalikankulunkulu pamoja na shule ya Sekondari ya Mpanda Ndogo.
Eng Manda alisema mradi huo ni wakisasa kwani mitambo yake ni ya kisasa na hata mashine zinawashwa kwa kutumia kompiyuta na mitambo hiyo ni yakudumu kwa muda mrefu wa miaka 25.
Kwa upande wa Wilaya ya Tanganyika wateja watakao taka kuwekewa umeme na shirika la umeme TANESCO watalipia kiasi cha shilingi elfu ishirini na saba tuu.
Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alisema kuwa mradi huo utakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa manispaa ya Mpanda kwani utaondoa tatizo la umeme lililokuwepo la kukatika mara kwa mara .
Aidha alilipongeza shirika la umeme TANESCO Mkoa wa Katavi kwa kuwa na mawasiliano mazuri na yakaribu kwa kutatua matizo ya wateja kwa haraka pindi yanapokuwa yametokea .
Diwani wa Kata ya Magamba Philipo Kalyalya alisema umeme huo utaleta manadiliko kwa Mkoa wa Katavi kwa wananchi wake kwa kuweza kujikomboa kiuchumi na kimaendeleo .
Kwani wafanyabiashara walikuwa wakishindwa kuanzisha viwanda vidogo kutokana na kutokuwepo kwa umeme wa uhakika hivyo sasa wanayofurusa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo .
Haidari Sumry Diwani wa Kata ya Makanyagio alisema pamoja na kupatikana kwa umeme huo wa ORIO vi vema Mkoa huo ukaunganishwa na umeme wa gredi ya Taifa kwani umeme wake ni wa gharama nafuu kuliko huo wa jeneleta .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment