Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kuwa bado haja zeeka na anazonguvu kubwa za kutowa mchango wa maendeleo ya Taifa licha ya kuwa ameisha sitaafu kazi Serikalini .
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati wa ibada ya juma pili kwenye misa ya pili iliofanyika katika Kanisa la Maria Imamakulata Jimbo Katoliki la Mpanda wakati alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa hilo kwenye misa ya ibada iliongozwa na Paroka wa Kanisa hilo Monsinyori George Kisapa .
Pinda alieleza kuwa bado anazo nguvu za kutosha kwa yeye kutowa mchango wa maendeleo kwa Taifa hili na kwenye jamii kutokana na hari ya nguvu alizonazo za afya ya kutosha .
Alisema mbali ya kuwa na nguvu za kutosha za kutowa mchango kwa Taifa pia bado anazonguvu za kutowa mchango pia kwenye Dini kwani yeye bado haja zeeka .
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliwaeleza waumini hao kuwa amefanya kazi Serikali kwa kipindi cha miaka 40 hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kipindi hicho chote alichofanya kazi Serikalini.
Alifafanua kuwa katika kipindi hicho cha utumishi akiwa Serikalini miaka ishirini na mbili amefanya kazi akiwa Ikulu na miaka 15 kazi ya siasa yaani Ubunge pamoja na miaka mitatu amefanya katika ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali .
Aliwaomba viongozi wa Dini wawaombee viongozi wa Serikali wawe na nguvu na afya za kuliongoza Taifa na pia waiombee nchi yetu amani na utulivu ulipo uzidi kuendelea .
Pinda aliwaka waumini wa Kanisa hilo kuwapeleka watoto wao kwenda kusoma kwenye Seminali ya Jimbo hilo inayoitwa Mtakatifu Paulo ili jimbo hilo liwe na mapadri wengi kwani yeye binafsi amevutiwa pia na matokeo ya ufaulu kwa kidato cha pili kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo Seminali hiyo imeshika nafasi ya kwanza kimkoa licha ya seminali hiyo kuanzishwa miaka mitatu iliyopita .
Paroka wa Kanisa hilo Monsinyori Gerge Kisapa alimshukuru waziri Mkuu huyo mstaafu kwa michango yake mbalimbali ya maendeleo aliyoitowa kwenye jamii na kwenye Kanisa wakati wa uongozi wake na baada ya uongozi wake .
Alisema naungana na Pinda kuwataka wazazi wawapeleke watoto wao kusoma seminalini kwani kusoma huko sio lazima mtu awe padri bali Seminali kunasaidia kupata viongozi bora kama Pinda aliyosoma katika Seminali ya Kaengesa lakini hakuwa padre na matunda yake yameonekana kwa Taifa letu la Tanzania .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment