.
Walter Mguluchuma .
Na Arine Temu .
Katavi.
Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Itenka katika Kata ya Itenka B Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Hapiam Salvatory 50 ameuwawa kikatili kwa kuchalangwa kwa mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kutenganishwa na kiwili wili.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa w Katavi Damas Nyanda aliwaeleza wandishi wa Habari kuwa tukio hilo la mauwji ya kikatili lilitokea hapo jana majira ya saa saba mchana .
Alisema kuwa siku hiyo ya tukio marehemu aliaga nyumbani kwake kuwa anakwenda mtoni kwenye shughuli zake alizokuwa akifanya kila siku za kuvua samaki kwenye mto Itenka uliopo Kijijini hapo .
Wakati akiwa njiani kuelekea mtoni marehemu alivamiwa na watu ambao walikuwa na mapanga na kumkatakata katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kuutenganisha kiwili wili na kichwa hadi kufariki Dunia hapo hapo .
Kamanda Nyanda alieleza kuwa baada ya wauwaji hao kufanya mauwaji ya kikatili na yakusikitisha waliondoka na kutokomea kusiko julikana na kuuwacha mwili wa Mwenyekiti huyo wa CCM ukiwa unagalagala barabarani .
Mwili wa marehemu huyo ulionwa na wananchi wawili ambao wakuwa wakipita kwenye eneo hilo na ndipo walipokwenda kutowa taarifa kwa uongozi wa Kijiji ambao nao walitowa taarifa kw jeshi la Polisi ambao walifika kwenye eneo hilo huku wakiongozwa na yeye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi na walikuta mwili wa marehemu huyo ukiwa umelazwa barabarani huku akiwa ameuwawa kikatili kwa kukatwa na mapanga.
Kamanda Nyanda alisema kabla ya tukio hilo marehemu huyo aliwahi kuandikiwa barua mbili miaka miwili iliyopita ya kutishiwa kuuwa na watu wasio julikana walikuwa wakimtuhumu kuwa ni mchawi .
Alieleza kuwa katika tukio hilo watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauwaji hayo ya mwenyekiti wa CCM na wanaendelea kuhojiwa kwa mahijiano zaidi .
Kamanda Damas Nyanda ametowa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai .
0 comments:
Post a Comment