Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Watu walio na ulemavu wa aina mbalimbali wanaoishi kwenye Mkoa wa Katavi wamemwahidi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Geralali Raphael Muhuga kuwa watashiriki kwa wingi kwenye sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo kwa mwaka huu zitazinduliwa Mkoani Katavi .
Watu hao wenye ulemavu walitowa ahadi hiyo hapo jana ambapo walijitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi uliofanyika kwenye ukumbi wa maji mjini Mpanda ambapo kila mlevu aliyehudhuria kwenye mkutano huo alipewa sare ya doti moja ya kitenge .
Katibu wa chama cha wenye ulemavu wa Mkoa wa Katavi Godfrey Sadala alisema wanaupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Katavi kwa kuweza kuwatambua na kuwashirikisha kwenye sherehe za uzinduzi wa mbio za mwenge kwa mwaka huu.
Alisema watu wene ulemavu wanapokuwa wamewezeshwa huweza kufanya shughuli kama watu wengine kwa kuwa Mkoa umewthamini na wao wanaheshimu kuthaminiwa na Serikali ya Mkoa wa Katavi .
Alieleza wamejipanga wao kama walemavu kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya uzinduzi wa mbio za mwenge Kitaifa zilizopangwa kuzinduliwa Mkoani hapo .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga aliweeleza watu hao wenye ulemavu kuwa mbio za Mwenge kwa mwaka huo zitazinduliwa Mkoani Katavi hapo Aprii 2 katia Uwanja mpya wa Mwenge uliopo katika Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda .
Aliwaeleza Mkoa umejipanga kuhakikisha makundi mbalimbali yanapata nafasi ya kushiriki kwenye uzinduzi huo na ndio maana wametenga sehemu maalumu wakakapo kaa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment