Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Serikali ya Mkoa wa Katavi imepiga marufuku kuanzia sasa uuzaji na utumiaji wa pombe za viroba katika maduka , Baa na kwenye maeneo mengine Mkoani Katavi na yeyote atakae bainika kukiuka agizo hilo halali atachukuliwa hatua kali za kisheria .
Agizo hilo lilitolewa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga mbele ya Wandishi wa Habari ofisini kwake.
Alisema kuanzia sasa anatowa tamko la kusitisha utumiaji ,uuzaji na ufungashaji wa pombe kali kwenye plastiki ndogo maarufu kama viroba na yeyote ambae atakiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine .
Na Mwananchi wote wa Mkoa wa Katavi wasisite kutowa taarifa juu ya watu watakao kaidi agizo hilo ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria .
Muhuga alisema matumizi ya pombe hizi yamesababisha athari mbalimbali hasa kwa vijana na yamechochea uharifu na kuongezeka kwa ajari za barabarani zinazotokana na Bodaboda hivyo kupelekea watu kuumia na wengine kupoteza maisha .
Pia katika baadhi ya maeneo Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari nao wamekuwa ni watumiaji wakubwa wa pombe za viroba .
Kuhusu madawa ya kulevya alieleza kuwa mpaka sasa Mkoa huu tayari unayo majina ya watu 12 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na uuzaji pamoja na usambaji ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa .
Alisema uchunguzi juu ya watu hao bado unaendelea na endapo watabainika watakamatwa na vyombo vya dola na kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.
mwisho
0 comments:
Post a Comment