Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Baraza la Maniwani la Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi limepisha uamuzi wa kutaifisha viwanja vya kujenga majengo ya makazi ya kuishi vilivyopo katika Manispaa hiyo ambavyo vimeshindwa kuendelezwa kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka 30 sasa.
Uamuzi huo uliulifanywa jana katika kikao cha Baraza hilo la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manspaa hiyo na kiicho ongozwa na Meya wa Manspaa ya Mpanda Willy Mbogo .
Uamuzi huo wa baraza la madiwani ulifuatia malalamiko ya Diwani wa Kata ya Kawajense Pius Buzumale kulalamikia uwepo wa masoko madogo madogo mengi ambayo sio rasmi kuwepo kwenye Manispaa hiyo kutokana na kuwepo kwa viwanja vingi vya makazi ambavyo vimeshindwa kuendelezwa .
Alilieza baraza hilo kuwa kitendo cha kuwepo kwa viwanja vingi vya makazi ambavyo vimeshindwa kuendelezawa ndio imekuwa chanzo cha watu kuamua kufanyia shughuli mbalimbali ambazo sio rasmi .
Diwani w Kata ya Makanyagio Haidari Sumry aliliaeleza baraza hilo kuwa kitendo cha kuwepo kwa shughuli katika maeneo ambayo sio rasmi kimekuwa kikisababisha Halmashauri hiyo ya Manspaa kupoteza mapato .
Meya wa Maspaa ya Mpanda Willy Mbogo alieleza kuwa eneo la mtaa wa Nsemlwa kichangani ndio ambalo wamwpanga kuanza nalo ambapo wapo baadhi ya watu wanamiliki viwanja kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 na wameshindwa kuviendeleza na baada ya kuvitaifisha viwanja hivyo watafanya zoezi hilo na kwenye mitaa mingine pia .
Alifafanua kuwa kwa wale watu ambao hawana muda mrefu toka walipopatiwa viwanja watawavumilia kidogo kwani watakao husika ni wale tuu walioshindwa kuendeleza kwa muda mrefu viwanja vyao ambao wengi wo wanazaidi ya miaka 30 .
Mbogo alisema utaratibu wa sheria inaeleza kuwa mtu anapopewa kiwanja anatakiwa ndani ya miezi sita awe ameisha anza kukiendeleza kiwanja chake hivyo kabla ya kuwataifisha viwanja hivyo watawapatia notisi ya kuwataka waviendeleze watakao shindwa kuendeleza watanyang-anywa .
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Geoge Nziyungu aliliambia baraza hilo kuwa Manispaa ya Mpanda imepanga kuanza kutoza kodo mbalimbali ambazo hapo awali zilikuwa hazitozwi ili kuongeza mapato ya Halmashauri .
Alizitaja baadhi ya kodi watakazo aza kutoza kuwa ni tozo kwa ajiri ya kupaki gari,tozo la kenye nyumba za kulala wageni ambapo kila mmiliki wa nyumba hizo anatakiwa kulipa ushuru wa asilimia 10 ya gharama ya kila chumba anachokuwa amelala mgini kwa siku .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment