Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wakazi wapatao zaidi ya 20,000 wakijiji cha Maji Moto Tarafa ya Mamba Wilayani Mlele Mkoani hapa wanalazimika kutembea umbali wa kilimeta saba kwenda Kata ya jirani ya Mamba kuchota maji ya kunywa kutoka na Kijiji hicho kukabiliwa na uhaba wa maji kwa kipindi kirefu .
Diwani wa Kata ya Maji Moto ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Nyansongo Serengeti aliwaambia jana wandishi wa Habari kuwa Kijiji hicho kimekuwa na uhaba wa maji yanayofaa kwa ajiri ya matumizi ya kunywa binadamu kutokana na maji yanayopatikana kijijini hapo kuwa na volikano .
Hili limekuwa ni tatizo kwa muda mrefu kwa wananchi wapatao 29,000 ambao wamekuwa wakilazimika kuangaika kufuata maji ya kunywa katika Kata ya jirani kwa kutumia usafiri wa baiskeli alisema .
Alieleza kuwa ndoo moja ya dumo moja la maji limekuwa likiuzwa kwa bei ya shilingi elfu moja hari ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wananchi wenye kipato kidogo walazimike kutumia maji pekee ya chemu chemu ya volikano ambayo ndio maji pekee yanayopatikana Kijijini hapo .
Diwani huyo alisema Halmashauri ya Mpimbwe imeisha anza mradi wa kujenga matanki mawili makubwa na kutandaza bomba za maji kutoka Kata ya Mamba hadi kwenye Kijiji hicho
.Lakini ni imani yangu kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano tatizo hilo la uhaba wa maji litakuwa limekwisha alisema .
Mkazi wa Kijiji hicho Salome Katumbo alisema maji ambayo yamekuwa yakipatikana kijijini hapo ni ya chemu chemu volikano na ambayo wamekuwa wakiyategemea ya mekuwa yakitoka huku yakiwa ni yamoto sana kanakwamba yametoka kuchemshwa kwenye moto
Hivyo maji hayo yamekuwa yakifaa tuu kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani kwa ajiri ya kufulia nguo na kupikia na kuoshea vyombo nasio kwa ajiri ya kunywa .
Juma Masanja kwa upande wake alieleza kuwa kutokana na yeye kuwa na familia ya watu wengi amekuwa akishindwa kununua dumo moja la maji kwa kiasi cha shilingi elfu moja kwa ajiri ya kuwa na kipato kidogo .
Hivyo amekuwa akichota maji kwenye chemu chemu na kuyahifadhi ndani ya nyumba na kuyasubilia kwa muda wa siku mbili yapowe ili waweze kuyatumia yeye na fmilia yake kwa matuzi ya kunywa kwani bila kufanya hivyo huwezi kuyanywa kutoka na kuwa ya moto sana kuliko hata chai .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment