Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limekamata silaha sita za kivita na Gobore 40 katika kipindi cha kuanzia januari mwaka jana hadi Desemba 2016 kutokana na juhudi za jeshi la Polisi kuimarisha ushirikiano mzuri na Wananchi katika kukabiliana na vitendo vya uharifu .
Hayo yalisemwa hapo jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda wakati alipokuwa akisoma taarifa mbele ya Wandishi wa Habari kuhusu hali ya kiusalama katika Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha mwaka 2016 kuhusu makosa yanayo husu uhalifu na makosa ya usalama barabarani .
Alisema katika kipindi cha mwaka jana Jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata jumla ya silaha saba ambazo ni Submachine Gun sita Shor gun moja pamoja na Gobore 40 ambapo katika kipindi hicho watuhumiwa 29 walikamatwa na kesi zao zipo katika hatua mbalmbali Mahakamani .
Katika kipindi cha mwaka 2016 silaha zilizosalimishwa kutoka mikononi mwa Wananchi i ni Submachine Gun nne na Gobore 81 mafanikio hayo yametokana na wananchi kuendelea kuelimika kupitia vikao mbalimbali vinavyoendelea kufanywa vya kuwaelimisha wananchi .
Kuhusu uhakiki wa silaha alisema katika kipindi cha mwaka jana silaha zilizohakikiwa zinazomilikiwa kwa mujibu wa sheria zilikuwa ni asilimia 74.63 na jeshi la polisi linaendelea kuwahimiza wananchi wnaomiliki silaha waendelee kujitokeza kuhakikiwa vinginevyo hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakao bainika kumiliki silaha psipo kahakikiwa hata kama wanauhalali na silaha hizo .
Kwa upande wa ajali Kamanda Nyanda alieleza kuwa matukio ya ajari kwa kipindi cha mwaka jana yalikuwa ni 65 ukilinganisha na ajari 112 zilizotokea mwaka 2015 hivyo kufanya kupungua kwa ajari 47 ambazo ni sawa asilimia 42.
Katika kipindi cha mwaka 2016 watu 34 walikufa kutokana na ajari za barabarani ukilinganisha na vifo vya watu 49 walikufa mwaka 2015 hivyo kufanya upungufu wa vifo 15 sawa na asilimia 31 na majeruhi kwa mwaka jana walikuwa ni 85 wakati mwaka 2015 majeruhi walikuwa ni 112.
Kamanda Yanda alisema matukio ya ajari yameweza kupungua Mkoani hapa kutokana na elimu inayotolewa ya kuelimishwa watumiaji wa vyombo vya moto kwa kukaguliwa mara kwa mara pamoja na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwani kauli mbiu yetu ilikuwa ni Hatutaki ajali , tunataka kuishi salama alisema Kamanda Nyanda .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment