Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Katavi KAREFA kImepata viongozi watakao kiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mine ijayo .
Uchaguzi wa kuwapata viongozi hao ulifanyika hapo jana katika ukumbi wa Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda na ulihudhuriwa na mjumbe wa kamati ya uchaguzi kutoka TFF Juma Lalika .
Makamu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya chama cha mpira wa miguu Walter Mguluchuma aliwatangazia wajumbe wa mkutano mkuu viongozi wapya wa chama hicho kuwa ni .
Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Emanuel Chaula alipata kura nane dhidi ya mpinzani wake kwenye nafasi hiyo Humud Sumry ambae alipata kura mbili . nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Robart Nyondo ambae alikuwa mgombea pekee w nafasi hiyo na alipata kura 10 katika ya kura 10 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano huo mkuu.
Nafasi ya Katibu mkuu ilichukuliwa na David Vianery ambae hakuwa na mpinzani yoyote na alipata kura kumi za ndio na katibu mkuu msaidizi alichaguliwa Idd Fumbo aliyepata kura za ndio kumi.
Mtunza hazina wa chama hicho alichaguliwa Evarsti Ntinda aliyepata kura nane za ndio na mbili za hapana mjumbe wa mkutano mkuu alichaguliwa Elias Milwano ambae alipata kuta tisa za ndio na moja ya hapana ambapo mwakilishi wa vilabu alichaguliwa Rahimu Said alipata kura kumi za ndio .
Wajumbe wa kamati tendaji ya chama cha mpira wa miguu waliochaguliwa ni Joseph Mlenda , Marcus Nazi na Brown Wilam ambao wote walipigiwa kura za ndio.
Uchaguzi huo ulivishirikisha vyama vitatu vya kutoka Manispaa ya Mpanda , chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Tanganyika na chama cha mpira wa miguu cha wanawake cha Mkoa wa Katavi .
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mwakilisha wa kamati ya uchaguzi kutoka TFF Juma Lalika alisema amefurahishwa na utaratibu ulifanyika kwenye uchaguzi huo kuanzia kwenye usahili hadi uchaguzi wenyewe .
Alisema vyama vingine navyo vinapaswa kuiga utaratibu wa uchaguzi wa KAREFA ambapo uchaguzi umefanyika kwa amani kubwa bila kuwepo na migogoro ya aina yoyote ile .
No comments:
Post a Comment