Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Hali ya kasi ya ugonjwa wa kipindupindu ulioukumba Tarafa ya Karema mwambao mwa Ziwa Tanganyika Wilaya mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi imepungua kutoka wagonjwa 88 hadi kufikia mg K onjwa mmoja .
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika aliwaambia wandishi wa Habari jana kasi hiyo ya ogonjwa wa kipindupindu ambao ulitokea kwenye Kata nne za Tarafa ya Karema umeweza kuthibitiwa kutona na juhudi kubwa zilizofanywa na wataalamu wa Afya.
Alisema ugonjwa huo ulitokea katika Kata za Ikola ,Kapamsenga Karema na Kasaga ntongwe ambao ulianza katikakti ya mwezi wa Dwsemba mwaka jana na watu 88 waliugua ugonjwa huo na watu wakatu kati yao walifariki Dunia.
Mhando alieleza kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na wataalamu wa afya wameweza kudhibiti ugonjwa huo na hadi kufikia jana alikuwa amebaki mgonjwa mmoja tuu katika kituo cha Karema .
Alisema kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo wa kipindupindu walilazimika kuweka vituo vinne kwenye Tarafa hiyo kwa ajiri ya kuwapokea wagonjwa na kuwapatia matibabu ambapo kila kata ilikuwa na kituo kimoja .
Alifafanua kuwa katika kipindi hicho cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu wameweka utaratibu wa kuwapulizia dawa watu wanaosafiri kabla ya kuingia kwenye sehemu ya Wilaya nyingine .
No comments:
Post a Comment