Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kuzuia na kupambana na Rushwa imepanga kusikiliza kero za Wananchi na kuwaelimisha Wananchi kuhusu mamlaka ya TAKUKURU na umuhimu wa kuripoti vitendo vya Rushwa na athari za Rushwa .
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Cristopha Nakua aliwaambia Wandishi wa Habari jana Ofisini kwake kuwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi itaanza maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kuzuia na kupambana na Rushwa hapo Desemba tano na watahiadhimisha Desemba 10.
Alieleza katika uzinduzi wa maadhimisho hapo Desemba 5 wamepanga kusikiliza kero za Wananchi ,kugawa machapisho na kuelimisha Wananchi kuhusu mamlaka ya TAKUKURU .
Pia watawaelimisha wananchi nanma ya kutowa taarifa na umuhimu wa kuripoti vitendo vya Rushwa na athari za Rushwa pamoja na kuwaelisha makosa ya rushwa .
Katika siku ya kilele cha maadhimisho hayo Desemba 10 TAKUKURU Mkoa wa Katavi imeandaa mdahalo kujadili maada zinazohusu rushwa na maadili walengwa wakubwa wakiwa ni Vijana na makundi mbalimbali .
Nakua alieleza siku hiyo ya maadhimisho ni siku maalumu kwa Serikali na jamii duniani kote kujitathimini wamefanya nini na wanafanya nini katika kuimarisha ,kuendeleza na kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa .
Allfafanua kuwa majukumu makubwa ya Takukuru ni kufanya uchunguzi na kuendesha mashitaka ,kuelimisha umma pamoja na kufanya tafiti na udhibiti ikizihusisha Taasisi za Serikali na mashirika ya umma na Taasisi binafsi katika mapambano dhidi ya rushwa na kuzishauri Taasisi husika ili kuziwezesha kubaini na kuzuia vitendo vya rushwa.
Alisema hapa Tanzania siku hiyo huitwa siku ya maadili Kitaifa na huadhimishwa desemba 10 kwa kuwa Desemba 9 ni sikukuu ya uhuru wa Taifa letu na mwaka huu Kitaifa yatafanyika Dares salaam.
MWISHO
1 comments:
Jamani update za katavi mbona kimya!? Sisi tulip mikoani huku tunatamani sana kupata updates
Post a Comment