Na Walter Mguluchuma
Katavi.
Waziri Mkuu msitaafu Mizengo Pinga ameitaka jamii ya Kitanzania kuachana na mila potofu za wanandugu kugombania mali za marehemu bali i waziache ili zitumiwe na mke wa marehemu na watoto aliowaacha marehemu .
Pinda aliyaeleza hayo juzi wakati wa mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kasansa Halmahauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Sixto Chalahani yaliofanyika juzi katika Kijiji cha Kasansa Tarafa ya Mamba .
Alisema kuwa ndugu wa marehemu wanapaswa kuachana na utamaduni huo wa kugombania mali za marehemu ambao unasababisha mjane wa marehemu na watoto kuhangaika badala yake kuhakikisha watoto walioachwa na marehemu wanaendelea na masomo hata kama mali hizo zitakuwa zimekwisha jamii iendelee kusaidia familia hiyo .
Alifafanua kuwa jamii ya kabila la Wapimbwe analotoka yeye Pinda mme anapofariki wanautamaduni wa ndugu wa upande wa mme kugawana mali za marehemu na kuwaacha mjane na watoto wa marehemu na kuwaacha mjane na watoto wa marehemu kuhangaika mitaani hatimae kwa waliokuwa wakisoma kushindwa kuendelea na masomo .
Wakati huo huo Pinda aliwataka wananchi wa Kata hiyo kuanza kujiandaa na uchaguzi mdogo kwa kufikilia nani atakuwa Diwani wao bora atakae weza kuendeleza aliyoacha marehemu Sixto Chalahani katika kipindi hiki kilicho baki .
Marehemu Sisto alikuwa ni Diwani wa Kata ya Kasansa toka mwaka 2010 hadi hapo mauti yalipomkuta tarehe 23 Agosti huko Sumbawanga katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa alikokwenda kupatiwa matibabu .
0 comments:
Post a Comment