Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu blog
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Yahaya Hussein ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi unakabiliwa na tatizo kubwa la mimba za utotoni zinazosababishwa na mila na destuli za baadhi ya makabila yanaishi katika Mkoa huo .
Alisema hayo hapo jana mbele ya wandishi wa Habari wakati alikuwa ofisini kwake wakati alipokuwa akitowa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Takwimu ya Taifa ya mwaka 2015 na 2016 DHS inayoonyesha Mkoa wa Katavi unaasimila 45 ya mimba za utotoni .
Dr Yahaya Hussein alieleza kuwa tatizo kubwa la wasichana kubeba mimba za utotoni lipo zaidi katika maeneo ya makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mpanda Mishamo Wilaya ya Tanganyika na zimekuwa zikisababishwa na mila na desturi za watu wanao ishi kwenye makazi hayo .
Alifafanua kuwa wakazi wanaoishi kwenye maeneo hayo ni wale wtu waliokuwa raia wa Nchi ya Burundi ambao hivi karibuni wamepewa urai wa Nchi ya Tanzania .
Alisema wamekuwa wakipokea akina mama wajawazito wengi katika Mkoa huu kwenye Hospitali na vituo vya Afya wanaoshindwa kujifungua kutoka kwenye maeneo hayo kutokana na pingamizi la uzazi unaosababishwa na wasichana kubeba mimba wakiwa na umri mdogo .
Hari hiyo ya kubeba mimba za utotoni imepelekea baadhi ya wajawazito kupoteza maisha yao wao na watoto wakati wa kujifungua na pia badhi yao wamekuwa wakipata ugonjwa wa fesitula .
Pia kiuchumi wamekuwa wakiongeza mzigo kwenye Serikali kwani gharama inayotumika wakati wanapokuwa wameshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kufanyiwa upasuaji huwa ni kubwa na pia gharama ya matibabu ya fesitula nayo ni kubwa pia ambapo serikali hubaba mzigo huo.
Mganga Mkuu huyo alieleza kuwa wasichana hao wenye umri mdogo wamekuwa wakiolewa na watu wenye umri mkubwa hari ambayo imekuwa ikiwalazimu waishi maisha ambayo hayalingani na umri wao .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisema wakazi wanaishi kwene Makazi ya Katumba na Mishamo ambao walikuwa ni Raia wa Nchi ya Burundi sela yao waliotoka nayo Burundi ni kushindana kuzaa hivyo wamekuwa wakizaliana bila kujali umri.
Hivyo Mkoa kuonekana unaidadi kubwa ya mimba za utotoni ni kutokana na maeneo hayo ambayo wazazi hawaini kitu cha ajabu msichana kubeba mimba akiwa na umri mdogo wao ni jambo la kawaida kutoka na mila zao
Alisema Mkoa umepanga kuhakikisha kila kiongozi anae kwenda kwenye maeneo hayo anawapatia elimu wananchi hao juu ya madhara ya mimba za utotoni na faida za uzazi wa mpango .
Nae Mratibu wa Marie Stopes Tanzania wa Mkoa wa Katavi Seif Mjuni alisema kuwa tatizo la mimba za utotoni limeenea kwenye makazi ya Katumba , Mishamo na Kata ya Maji moto Wilayani Mlele wanako ishi jamii ya wafugaji .
Alisema mbali ya tatizo la mimba za utotoni kuchangiwa na mila na destuli tatizo jingine linalosababisha ni uwelewa mdogo wa wananchi kuhusu afya ya uzazi .
Ndio maana Marie Stopes katika Mkoa wa Katavi wameweka utaratibu wa kufika kila Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi na kutowa elimu kwa muda wa siku mbili kila mwezi juu ya elimu ya uzazi .
0 comments:
Post a Comment