Monday, July 18, 2016

WALIMU WANAWAKE WATAKIWA KUJIENDELEZA KITAALUMA .


   Na  Walter   Mguluchuma 
      Katavi  yetu blog.
Mjumbe  wa   Kamati  ya   utendaji     Taifa    Mkoa  wa   Katavi wa  Chama  cha  walimu  CWT    Costantine  Marcely  amewataka   Walimu  wanawake  wajiendeleze  kitaaluma , kiuchumi   na kujishirikisha   katika   vyombo   mbalimbali  vya  maamuzi   katika  sehemu za kazi   ndani ya CWT   Serikalini  na  kwenye  taasisi  nyingine .
  Wito  huo  aliutowa  hapo  jana   wakati  alikuwa  akifungua  mafunzo  ya  kuwajengea  uwezo     walimu   Wanawake  viongozi  wa   CWT  wa kitengo  cha  Wanawake     yaliofanyika  katika   ukumbi  wa   chama  hicho na  kuwashirikisha  viongozi  wanawake  wa  CWT  kutoka   Halmashauri  zote  za  Mkoa  wa  Katavi .
 Alisema  moja  ya  majukumu walionayo  walimu  wanawake     viongozi  katika    sehemu  zao  za  kazi  ni  kuwahimiza   walimu  Wanawake   wajiendeleze   kitaaluma , kiuchumi  na kujishirikisha  katika  vyombo  mbalimbali   vyenye  maamuzi   sehemu ya  kazi   ndani ya  CWT Serikalini ,  vyama  vya  siasa   na   kwenye  taasisi  nyingine .
Marcely  alieleza  kuwa  Walimu  wanawake  wamekuwa  hawajitozi  kwenye  maswala  ya  kugombea   nafasi  mbalimbali  za  uongozi   ndani ya   chama   hicho   kutokana  na  kutojiamini  kuwa  wanaweze  hivyo     ni  wajibu  wa  walimu   viongozi  wanawake   wakawahamasisha  kugombea  nafasi  mbalimbali  pindi  zinapokuwa  zimetokea .
Katibu  wa   CWT wa   Mkoa  wa   Katavi    Lucy    Masegenya   alieleza  liwaeleza    washiriki  wa  mafunzo  hayo ya  siku  moja   kuwa  takwimu    mbalimbali    katika  Sekta    za  elimu    ,  ajira    na  uongozi   zinaonyesha   na  kuthibitisha   kwamba   wanawake   hawana   fursa   na  haki  sawa   kama  ilivyo  kwa wanaume  katika  utoaji wa  maamuzi   na   uwakilishi   katika  vyombo  mbalimbali .
Alisema    juhudi  za    shirikisho    la  vyama  vya   wafanyakazi   Tanzania   TUCTA  na  vyama   shirikishi  kikiwemo  chama  cha  Walimu    Tanzania   katika  kutatua   matatizo   yanayowakabili Wafanyakazi    zimeonyesha   kuwa   wanawake   wanakabiliwa  na    changamoto  nyingi .
  Masegenya   alizitaja  baadhi ya   changamoto  kuwa  ni   tamaduni  zilizopitwa  na  wakati   zinazombagua   mwanamke  na  kumnyima   fursa  sawa   katika   jamii   kama  vile  kutorusiwa  kumiliki   rasilimali   za    familia nyinginezo .
Changamoto  nyingine  ni   ubaguzi  wa  kijinsia   katika  ajira   na   fursa   mbalimbali   katika   jamii   kama    vile   elimu   na  uongozi .
Nae   Mshiriki  wa  mafunzo  hayo  mwalimu   Coleta  Mathias   alisema   walimu  wanawake  wamekuwa  wakipata  wakati mgumu kuongoza  kwenye  maeneo ya  shule  kutokana   na  baadhi ya  walimu   wanaume   kutokubali  kuwatambua  na  wamekuwa   wakishindwa kupata  ushirikiano   wa kutoka  kwa  walimu  wenzao wa kike   kutoka  na  tabia ya kutopendana  kwa walimu wa kike kwa   wakike .
 Pia    baadhi ya  walimu   wanaume  wamekuwa  hawapendi  kukaa  na  walimu wa  kike  kwenye  shule  moja  na  matokeo yake wamekuwa  wakiwafanyizia   visa  mbalimbali  walimu wa  kike .
Mwalimu  Bestlila   Msafiri   alieleza  kuwa  kwenye   taasisi   mbalimbali  ambazo wanawake  wamekuwa  wakipangiwa  kufanya  kazi   baadi  yao  wanapopangiwa   kufanya  kazi  maeneo ya  vijijini  wamekuwa wakiona  hawezi  kwenda  kufanya    kazi  huko  na  matokeo yake  wamekuwa  wakitowa   rushwa  ya  ngono  ili  wapangiwe  vituo  vya  kazi  za  mijini.
Alieleza  ilikuondokana  na  rushwa  ya   ngono    ni   vizuri  wanapokuwa  wamepangiwa  kufanya  kazi   vijijini   waache   tabia  ya  kwenda  kuomba  wapangiwe  vituo  vya  kazi  vya  mjini  tuu wajione  kuwa  wanawake  wanaweza  kufanya  kazi  sehemu  yoyote  ile  ya  vijiji  na  mjini  kwani  wanawake  wanaweza ,

No comments:

Post a Comment