Na Walter Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi inampango wa kubinafufisha huduma ya usafishaji na utunzaji wa mazingira katika maeneo yote ya Manispaa ya Mpanda ili kuboresha zaidi usafi wa Manispaa ya .Mpanda.
Hayo yalisemwa hapo juzi na Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo wakati alipokuwa akilihubia Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda .
Alilieleza Baraza hilo Manispaa imepanga kubinafusisha shughuli za usafishaji na utunzaji wa mazingira kwa Makampuni na mawakala ambao watapewa ushirikiano wa karibu katika kufanya kazi hizo na uongozi wa Serikali za Mitaa, vitongoji na Kata .
Lengo la utaratibu huo wa ubinafishaji wa usafi katika maeneo ya Mitaa, kuishi biahara na maeneo ya kufanyia kazi ni kuhakikisha kuwa mazingira ya manispaa yanakuwa safi wakati wote na rafiki kwa jamii kwa kiwango cha asilimia 97.
Mbogo alifafanua kuwa mawakala watagawanyishwa katika makundi mbalimbali ambapo wakala mmoja atahusika na huduma ya utoaji na udhibiti wa taka ngumu .
Wakala mwingine atahusika kwa ajiri ya utozaji wa faini isiyozidi Tsh 50-000 kwenye maeneo yatakayobainika kuwa ni machafu ya ofisi , nyumba za kuishi ,mapagala na kwenye viwanja na watu wanao zalisha madampo .
Pia wakala mwingine atahusika na kuunda kikoso kazi cha askari wa manispaa kwa ajiri ya kukamata mifugo kama vile nguruwe , mbuzi na ng-ombe watakao kuwa wanazurula ovyo na watatozwa faini kati ya Tsh 10-000 na Tsh 20,000.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Lauteli Kanoni alieleza kwenye baraza hilo kuwa Manispaa hiyo imekuwa ni washindi wa pili katika utunzaji na usafi wa mazingira kwa Halmashauri zote nchini za Manispaa .
Alisema utarabibu huo wa ubinasishaji utaifanya manispaa hiyo iweze kufanya vizuri zaidi katika swala la usafi wa mazingira na kuifanya hapo mwakani iweze kuwa ya kwanza.
MWISHO
No comments:
Post a Comment