Na Walter Mguluchuma
Katavi
Wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Mkoa wa Katavi wameiomba Serikali kusiliza kilio chao cha muda mrefu cha kutengewa maeneo wachimbaji wadogo kwa ajiri ya uchimbaji wa madini ya Dhahabu .
Maombi hayo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu yalitolewa jana na wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi kwenye Risara yao iliyosomwa na mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wa dogo wa Mkoa wa Katavi Willy Mbogo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medadi Kalemani kwenye kikao baina yao na Naibu Waziri kilichofanyika katika Hotel ya Lyamba Lyamfipa mjini hapa .
Mbogo alisema wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi wanayomasikitiko makubwa sana kuona Wizara ya Nishati na Madini imeshindwa kufatilia ombi lao la muda mrefu waliloomba kutengewa maeneo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Mkoa wa Katavi .
Alieleza wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Mkoa wa Katavi hawajatengewa eneo la uchimbaji pamoja na maombi yao kadhaa walioba kwa wizara hiyo .
Eneo wanaloliomba wachimbaji wadogo iliwafanyie shughuli zao lilikuwa linamilikwa na Kampuni ya GBA ambalo kwa sasa liko wazi na lina maombi ya Kampuni ya Kijani Investment inayomilikiwa na mwanasiasa maarufu Crisanti Mzindakaya.
Mbogo alisema wachimbaji wadogo wanazosababu za msingi za kuomba wapatiwe eneo hilo lililoombwa na Kampuni ya Kijana Investment kwani mmiliki wa Kampuni hiyo ndiye mmiliki wa Kampuni za Crystal Mkwamba ,Mkwamba minerals, GBA na sasa Kijani Investment.
Hivyo kampuni hiyo imekuwa ikifanya ujanja wa kubadil majina ya Kampuni kila mara na kuhodhi maeneo yote yenye mashapo ya dhahabu Mkoani Katavi toka mwaka 1998 bila kuanzisha mgodi hata mmoja .
Alifafanua kuwa endapo wachimbaji wadogo watanyimwa eneo hilo wanaloliomba na Wizara ya Nishati na madini ikampatia mwekezaji mkubwa atapata tabu kuanzisha mgodi huo kwa sababu ya mwingiliano wa kuwepo na leseni ndogo nyingi kwenye eneo hilo hivyo atalazimika kuwafukuza wakazi wengi wa eneo hilo na huduma za jamii zilizopo za shule na Zahanati zitafungwa .
Pia wamaiomba Wizara hiyo imemalize mgogoro baina ya wachimbaji wadogo 32 walipewa leseni za kuchimba katika eneo la Kampuni ambalo eneo hilo jeshi la Wananchi wa Tanzania linadai kuwa ni eneo lao na limewasimamisha wachimbaji hao kufanya shughuli kwenye eneo hilo licha ya kuwa na leseni za kuchimba .
Naibu Waziri Dk kelemani aliwaeleza wachimbaji hao kuwa Wizara inaendelea na mazungumzo na Kampuni ya Kijani Investment ilikuona uwezekana na kupunguza eneo hilo la kugawiwa wachimbaji wadogo na yatari wameisha kaa na mzee huyo alisema Naibu Waziri .
Alisema Wzara imepanga kuyachukua maeneo yote ambayo walikuwa wamepewa watu kufanya utafiti na washindwa kuyaendeleza maeneo hayo yakisha chukuliwa watagawiwa wachimbaji wagogo .
Alisema Kampuni hiyo imeomba maneo mengi ya uchimbaji wakati wachimbaji wadogo wako wengi hari hiyo imesababisha eneo lililopo kuwa halitoshi kwa wachimbaji wadogo .
Serikali inatambua sana mchango wa wachimbaji wadogo kwani wao ndio huwa ndio wanakuwa wavumbuzi wa kwanza wa madini katika maeneo yanayopatikana madini.
Kuhusu mgogoro wa wachimbaji wagodo na Jeshi la wananchi alisema Serikali itaangalia kama kuna manufaa kwa Taifa itakayopatikana kutokana na madini yaliyopo eneo la Kampuni jeshi wanaweza kuondolewa kama walivyohamisha Gereza Mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment