Tuesday, July 19, 2016

HATARI: MLINZI WA KAMPUNI YA ULINZI AJINGONGA KWA KUTUMIA SHATI LAKE

 .
       Na   Walter  Mguluchuma .
             Katavi .  yetu blog
  Mlinzi wa  Kampuni ya  Ulizi ya  Imala  Secuty  Guard  Samwel  Alkado 39 amekutwa  akiwa  amejingonga   ndani ya  chumba  chake katika   Mtaa wa   Mji wa  Zamani  Manispaa ya  Mpanda kwa kutumia   shati .
 Kwa  mujibu wa  Mwenyekiti wa  Mtaa wa   Mji wa  Zamani  Magret  John  tukio  hilo  lilitokea  hapo  jana   majira  ya  saa   kumi  na  moja  na   nusu   alfajiri  katika   Mtaa wa   Mji wa   Zamani   ndani ya  chumba  alichokuwa  akiishi   marehemu   Samwel.
Kabla ya  tukio  hilo  marehemu alikuwa  akisumbuliwa  na  maradhi  ya  mara kwa  mara   hari  ambayo ilimfanye  aende   hospitali  ya  Wilaya  kwa   ajiri  ya  kufanyiwa  uchunguzi wa  vipimo mbalimbali .
Mwenyekiti  huyo wa  Mtaa  aliwaeleza  waandishi wa  Habari  baada ya  kufanyiwa uchunguzi wa  vipimo  ndipo   marehemu  aligundulika  akiwa  na virusi vya  VVU.
 Alisema  baada ya  kupatiwa  majibu  hayo  marehemu  alianza kuchanganyikiwa   hari  ambayo ilimfanya   hata  utendaji wake wa  kazi  uzoleta  na  kumfanya  mwajiri  wake achukue  uamuzi  wa  kumerudisha  kwao   mjini   Sumbawanga  Mkoani   Rukwa .
Ndipo   apo  jana   kiongozi wa  Kampuni  hiyo ya  ulinzi  aliyejulikana  kwa  jina  la  Omary  Ismaili alipofika  kwenye  nyumba aliyokuwa  amepanga  marehemu kwa  lengo la kumwamsha  kwa  ajiri ya  safari  hiyo  na  alipompigia  hodi  hakuweza  kuitika  hari  ambayo  ilimfanya    apate  shaka  na kuwaamsha  wapangaji  wengine.
Kitungulu    alisema  wapangaji wenzake  walijaribu  kubisha  hodi lakini  hakukuwa  na  dalili  zozote  za  marehemu  kuamka  hari  ambayo  iliwafanya  waende kutowa  taarifa  kwa  viongozi wa  mtaa wa  Mji wa   zamani .
Viongozi wa  mtaa wa  Mji wa  Zamani  baada ya  kufika  kwenye  eneo  hilo waliamuru  mlango wa  chumba  hicho  uvunjwe  ndipo walipovunja  mlango n a  walipoingia  ndani walikuta  marehemu  akiwa  amejinyonga kwa kutumia  shati  lake  huku  akiwa uchi.
Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi  Damas  Nyanda  amethibitisha kutokea kwa kifo  hicho  na  jeshi la polisi  Mkoa wa  Katavi  linaendelea  na  uchunguzi  zaidi  wa tukio  hilo .
Mwili wa  Marehemu  Samwel  Alkado umehifadhiwa  katika  chumba  cha maiti  katika  Hospitali ya  Wilaya ya  Mpanda kwa ajiri ya uchunguzi wa kidaktari.

No comments:

Post a Comment