Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
MKUU wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi Rachel Kasanda amewapiga marufuku watumishi wa umma katika wilaya hiyo kuacha mara moja tabia ya kusafirisha nyaraka za serikali katika njia ambazo hazitambuliki kiserikali kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Akizungumza na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano uliopo shule ya sekondari Inyonga iliopo wilayani humo ambapo pia alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa watumishi hao.
Alisema kuwa wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kama Whatsup na barua pepe ambazo serikali haijaelekeza kuzitumia wao wamekuwa wakituma nyaraka za serikali kupitia njia hizo.
Alisema kuwa kunawakati utakuta kuna nyaraka zinahitajika wizarani haraka unakuta mtumishi anaamua kuipiga picha kwa simu nyaraka hiyo na kumtumia mtumishi mwenzake wizarani kwa njia ya whatsup.
Kasanda alisema kufanya hivyo ni makosa na watumishi wanapaswa kutambua kuwa baadhi ya nyaraka za serikali zinakuwa ni siri hivyo njia hizo hazina usiri kwani kunahofu hata ya mataifa mengine kudukua siri za serikali yetu.
Aliwaambia kuwa nyaraka zote ni lazima zitumwe kwa kutumia barua pepe zilizo idhinishwa na serikali na si vinginevyo.
Aidha mkuu huyo wa wilaya aliwataka watumishi hao kubadirika na kujituma katika kuwatumikia wananchi kwani watambue kuwa serikali ya awamu ya tano imeamua kushuka chini na kuwajali wananchi kwani ndiyo waajiri wao namba moja.
Alisema kuwa rais John Magufuli amemtuma yeye kumwakilisha wilayani
humo hivyo hayupo tayari kumwangusha na atafanya kila liwezekanalo
kuhakikisha anatatua changamoto za wananchi.
No comments:
Post a Comment