Na Walter Mguluchuma.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Rachael Kassanda ametowa agizo kwa Watumishi wa Wilaya hiyo kutofanya kazi kwa mazowea hari ambayo inasababisha Wananchi kutopata huduma zao kikamilifu na kwa wakati.
Mkuu huyo wa Wilaya alitowa agizo hilo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele katika kikao cha utambulisho wake kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Inyonga.
Alisema ili mtumishi aweze kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi kwa wakati muafaka ni lazima kuwe na mpango kazi utakao mwongoza katika kutekeleza shughuli za kiutumishi na ambao utakuwa dira ya kuhakikisha sera ya hapa kazi tu inazingatiwa.
Alifafanua kuwa watumishi wengi wakuwa hawatekelezi majukumu yao ya kazi ipasavyo kwa ajiri ya tabia ya kufanya kazi kwa mazoea hivyo watumishi wanaofana kazi kwa mazoea waache mara moja .
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya Kassanda aliwataka watumishi kusafirisha nyaraka za Serikali kwa njia sahihi na inayotambulika Kiserikali ili kuhakikisha usalama wa nyaraka husika na utunzaji wa siri za Serikali kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kiutumishi .
Alisema kumekuwa na mazoea ya watumishi wa Serikali kutumiana nyaraka za Serikali kwa njia ambazo sio halali ikiwa ni pamoja na barua pepe ambazo hazina umiliki wa Serikali ambazo ni yahoo, Gmail Hotmail Rocketmail,na Whatsaap.
Hivyo mtumishi yoyote wa Serikali ambae atasafirisha nyaraka za Serikali katika Wilaya yake ya Mlele kwa njia isiyo sahihi atahakikisha anachukuliwa hatua kali za kinidhamu za kiutumishi .
0 comments:
Post a Comment