Home » » ZAIDI YA NG’OMBE 5840 ZAUAWA KWA KUPIGWA RISASI KATAVI.

ZAIDI YA NG’OMBE 5840 ZAUAWA KWA KUPIGWA RISASI KATAVI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Walter   Mguluchuma na  Arine  Temu,Katavi.

Baadhi ya Wafugaji wa wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wameilalamikia
serikali ya Tanzania kwa kushindwa kutenga maeneo ya kuchungia ikiwa
pamoja na kuruhu Mifugo kuawa kikatili.
Wakizungumza  Jana kwa masikitiko mbele ya Katibu Mkuu wa chama cha wafugaji

Tanzania (CCWT) Magembe Nkonosenema Kwenye Mkutano uliofanyika  Kijiji
cha Mkuyuni Kata ya Majimoto Wilaya Mlele Mkoani humo Walisema zaidi
ya Ng’ombe 5840 wamekufa kwa kupigwa risasi ndani ya mwaka 2013 hadi
2015 kutokana na kuwa ndani ya eneo la Rukwa Rukwate lililotengwa kama
eneo la akiba la hifadhi.

Wafugaji hao Walisema kuwa kitendo cha kuua mifugo yao kwa namna hiyo
hakikubaliki Ambapo walihoji kwa maswari kuwa ni kwa  Mamlaka gani,
naya nani ikiwa ya sheria gani?,Yanatumika kutekeleza mauaji hayo.

‘’Ndugu Katibu,Niuonevu na Udharimu mkubwa tunaofanyiwa Wafugaji wa
Nchi hii.Tunafanya kazi kwa bidii kupata Mifugo ili iweze kukidhi
mahitaji ya kifamilia na kibiashara Lakini inauliwa hovyo’’Walisema
Semi  Maletwa na Elisesi Ng’anza walio uliwa zaidi ya Ng’ombe mia
tano.

Aidha,Wafugaji hao walizidi  kuitupia  lawama serikali kuwa chanzo cha
tatizo hilo kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki za kudhibiti Mauaji
ya mifugo yao ikiwa pamoja na kutenga haraka maeneo ya kuchugia licha
ya kuchangia asilimia nne ya pato zima la serikali.

Sanjali na hayo Walisema kuwa Wafugaji wamekuwa wakikamatwa na
Maaskali wa hifadhi na kupigwa,Kuteswa vikali ikiwa pamoja na kutozwa
faini za juu zinazofikia Mil 15 hadi Mil 20 nakutokuwa linganifu na
idadi ya Mifugo wanayo ikimata  na kunyimwa Stakabadhi za malipo ya
faini hizo.

Naye  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tazania(CCWT) Magembe
Nkonosenema alisema Matatizo yanayo wakabili wafugaji ameanza
kuyatafutia ufumbuzi ikiwa ni kuyatolea taarifa kwa Waziri mwenye
dhamana na kufikia sasa tayari Serikali imeanza kufanya juhudi za
kutafuta maeneo ya kuchungia ikiwa zoezi hili limepewa chama cha
wafugaji kuliongoza ikishirikiana na wadau wengine wa Mazingira.

Nkonosenema pia alifafanua  umuhimu wa Wafugaji nchini kutoa
kipaombele katika suala la elimu kwa kuwasomesha watoto wao ili wawe
chachu ya mabadiliko katika familia zao za kifugaji kwa kuleta
maendeleo na kuwatetea pindi wanapopatwa na matatizo ya kisheria.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa