Na Walter Mguluchuma
Katavi
Zaidi ya shilingi milioni 56 zimerejeshwa Mkoani Katavi hadi sasa katika ya zaidi ya shilingi Milioni 240.3 zilizolipwa kama mishahara hewa katika Mkoa wa Katavi kiasi hicho kilichorejeshwa ni sawa na asilimia 23.3.
Fedha hizo zimerejeshwa kufuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga alilolitowa kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Katavi la kuwataka wahakikishe fedha zote walizolipwa watumishi hewa 46 waliobainika katika Mkoa wa Katavi zinarejeshwa Serikalini .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu aliwaambia Waandishi wa Habari jana ofisini kwake kuwa hadi sasa kiasi cha shilingi 56,1o2,900 zimerejeshwa kati ya shilingi milioni 240,369,257 zilizolipwa kama mishahara hewa katika Mkoa wa Katavi kiasi hicho ambacho ni sawa na asilimia 23.34.
Alisema hadi kufikia Mei 4 mwaka huu Mkoa wa Katavi ulikuwa na idadi ya watumishi hewa 46 ambao walibainika wakiendelea kuchukua mishahara wakati hawasitahili na kuitia hasa Serikali kiasi cha shilingi Milioni 200,792,448.
Alifafanua kuwa watumishi waliokufa lakini walikuwa wakiendelea kulipwa mishahara walibainika watano, watumishi waliostaafu 19, walioacha kazi kwa hiari lakini walikuwa wakilipwa alibanika mmoja , waliokuwa na mishahara miwili wawili, watumishi ambao ni watoro sugu na hawapo vituoni 13.
Watumishi waliokuwa na vyeti vya kugushi ambao walikimbia na kutokomea kusiko julikana baada ya timu aliyoiunda kuanza kufanya kazi ni watatu na watumishi waliofukuzwa kazi na kuendelea kulipwa mishahara ni watatu .
Meja Jenerali Mstaafu Muhuga alisema Manispaa ya Mpanda ambayo ilibainika kuwa na idadi ya watumishi hewa 16 hadi june 20 ilikuwa imerejesha kiasi cha shilingi Milioni 24,841,899 kati ya Tsh 69,917216, Halmashauri ya Nsimbo yenye watumishi hewa 11 hadi sasa imerudisha Tsh 9,306,800 kati ya Tsh 90,661,880.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda walibainika watumishi hewa tisa na wamerejesha kiasi cha shilingi milioni 12,674,201 kati ya shilingi milioni 33,759,041 na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele yenye watumishi hewa tisa wamerejesha kiasi cha shilingi milioni 9,280,000 kati ya shilingi milioni 46,031,120.
Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa kuhusu watumishi hewa 15 ambao taarifa zao zina utata , uchunguzi bado unaendelea ambapo TAKUKURU inasaidia fuatilia ili kuhakikisha taarifa muhimu ambazo tume aliyoiunda ilishindwa kuzipata kwa baadhi ya watumishi kutokana na taratibu za kisheria katika Benki ya NMB zinapatikana
Muhuga alisema zoezi hilo la urejeshwaji wa fedha za mishahara hewa bado linaendelea katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi na watumishi hewa waliobainika katika Mkoa wa Katavi tayari wamefutwa kwenye orodha ya watumishi wanaolipwa mishahara .
Na baada ya kukamilika kwa urejeshwaji huo ndipo maafisa utumishi wote ambao wakakao bainika kuhusika na mishahara hewa watachukuliwa hatua za kinidhamu za kiutumishi pamoja na watumishi walioshirikiana nao .
0 comments:
Post a Comment