Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Wanawake na wasichana wanaofanya biashara katika masoko ya Manispaa ya Mpanda wamepatiwa mafunzo ya kukuza sauti na kuimarisha haki za mwanamke na wasichana kushiriki nafasi za uongozi katika maeneo ya masoko wanakofanyia kazi na wanako ishi .
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na shirika la Tanzania Community Media organization TACOMO yalifanyika jana katika ukumbi wa Mtakatifu Maria Mjini Mpanda.
Kiongozi mkuu wa shirika hilo lisilo la Kiserikali lenye makao yake makuu Jijini Mbeya Gordon Kalulunga alisema mafunzo hayo yanalengo la kuwaelimisha wanawake na wasichana watambue haki yao ya kuwania uongozi katika sehemu zao wanazofanyia kazi na wanako ishi pia walipatiwa mafunzo ya ujasilimali kwa wanawake .
Alisema wanawake wamekuwa hawajitokezi kuwania nafasi mbalimbali kwenye maeneo wanayofanyia kazi na wanako ishi kutokana na kuwa waoga wakati uongozi ni kalama ndio maana TACOMO imeamua kutowa mafunzo hayo ili wanawake na wasichana watambue haki yao ya kuwania uongozi katika sehemu zao wanazofanyia kazi na wanako ishi .
Afisa Maendeleo jamii wa Kata za Kashaulili na Majengo Imelda Mkama alieleza kuwa mafunzo hayo waliopatiwa wanawake na wasichana yatawafanya ushiriki wa wanawake kuwa mkubwa katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi .
Kuhusu ujasilimali afisa huyo wa Maendeleo ya jamii alieleza kuwa mjasilamali lazima awe ni mtu ambae si wakukata tama na awe ni mtu mbunifu wa shughuli za kufanya na asiwe mtu wa kuiga biashara ya mtu mwingine.
Salome Mwanandeje mshiriki wa mafunzo hayo alisema wanawake wengi wamekuwa hawajitokezi kuwania nafasi za uongozi kwa kuwa huwa wanajihisi kuwa wakigommbea watashindwa wakati wanawake wanaweza.
Alisema wanawake wamekuwa hawagombei kwa wingi nafasi za uongozi kwa kuwa huwa awajiamini na pia wamekuwa hawapendani wao kwa wao badala ya kutiana moyo wamekuwa wakikatishana tama.
Juliana Nyanda alisema elimu kwa jamii bado ipo chini kwenye uelewa wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa wanawake .
Nae Asha Tende alieleza kuwa wamekuwa wakikatishwa tama kugombea nafasi za uongozi kutokana na baadhi ya makabila yamekuwa na tabia hayataki kutawaliwa na wanawake.
Washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja yalwashirikisha wanawake na wasichana wanaofanya biashara katika masoko ya Buzogwe, Mpandahotel, Makanyagio, Soko kuu na soko la matunda la Kawajense yalioko katika Manispaa ya Mpanda.
No comments:
Post a Comment