Wednesday, June 15, 2016

JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI NGOZI YA NYUMBU ,SIMBA NA CHUI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Walter  Mguluchuma  na  Irine  Temu
                Katavi yetu Blog
Mahakama  ya  Wilaya  ya  Mpanda  Mkoa   wa  Katavi  imemuhukumu   Kasanzu  Kwimba   Mkazi wa  Kijiji  cha  Maduu  Wilaya  ya  Mlele  kifungo  cha  miaka  20  jela baada ya kupatikana  na  hatia ya kupatikana  na  nyara za  Serikali   zenye  thamani ya  zaidi  ya  Shilingi  Milioni  15.

  Hukumu  hiyo  ilitolewa  jana  na  Hakimu  Mkazi    Mfawidhi  wa  Mahakama ya  Wilaya  ya  Mpanda  Chiganga  Ntengwa  baada  ya  kulidhika  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani  hapo     na upande wa  mashitaka .
 Awali  katika  kesi  hiyo  Mwanasheria  wa  Mkoa  wa   Katavi   Jamila  Mziray   alidai Mahakamani  hapo  kuwa  mthumiwa   alitenda  kosa   hilo   hapo  mei     27  mwaka   jana   katika   Kijiji  cha    Maduu  Wilaya  Mlele.

 Alidai kuwa  siku  hiyo ya  tukio  mtuhumiwa  alikamatwa   nyumbani    kwake  akiwa  na   nyara  mbalimbali za  Serikali  akiwa  amezihifadhi  ndani ya   nyumba yake   zenye    thamani  ya   shilingi  Milioni   kumi  na   tano  na   laki  saba .

Mziray  alizitaja   Mahakamani  hapo    nyara  alizokamatwa  nazo   mthumiwa  kuwa  ni   ngozi  ya  chui moja , ngozi  ya  Simba samba moja    ngozi ya   nyumbo  moja  na   ngozi   paka  pori .
   Mwanasheria  huyo  aliiambia   Mahakama  kuwa  mtuhumiwa  alikamatwa   baada  ya   jeshi  la  polisi  na   askari wa    Hifadhi  ya  Taaifa   ya  Katavi  kupata  taarifa  kuwa   mtuhumiwa  anamiliki  nyara  za  Serikali   kinyume  cha  sheria   na    ndipo  walipomfanyia upekuzi waliweza kumkuta   na  nyara  hizo za  Serikali.

Hakimu  Mkazi   Mfawidhi   Chigamga    Ntengwa  akisoma   hukumu  hiyo  aliieleza  kuwa    kutoka  na  ushahidi  uliotolewa Mahakamani  hapo  Mahakama  imeridhika  na  ushahidi uliotolewa   mahakamani   ambapo  mshitakiwa  amepatikana   na    hatia.

  Alieleza  kkutokana   na  kupatikana  na   kosa  hilo  mahakama  inatowa  adhabu kwa  mshitakiwa  ya kifungu  cha     sheria    Namba  235   ya  marekebisho  ya  sheria  ya  mwaka  2002.
  Hivyo  Mahakama  imemuhukumu  Kasanzu   Maduu   kutumikia  kifungo   cha  miaka  ishirini  jela kuanzia  jana  ili  ikaweze   kuwa na   tabia   njema   akimaliza   kifungo   chake  kwenye   jamii

No comments:

Post a Comment