Baadhi ya wafugaji wa Kijiji cha Katambike Kata ya ugala Wilata ya Mlele wakitowa malalamiko yao ya kuwashutumu watumishi wa Maliasili wanavyo wanyanyaa wafugaji malalamiko hayo waliyatowa hapo jana kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Maji Mjini hapa kwa Katibu Mkuu wa chama cha wa wafugaji Tanzania Magembe Nkonosenema ambae hayupo pichani
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Thiodela Kisesa akiwahutubia wafugaji wa Mkoa wa Katavi katika kikao kilichofanyika jana katika ukumbi wa idara ya maji ambapo aliwataka watumishi wa idara ya maliasili kufanya kazi kwa kufuata utaratibu na heria na wafugaji waache kuishi maeneo ambayo hayasitahili waishi .
Picha Na Walter Mguluchuma Katavi yetu Blog
N a Walter Mguluchuma
Katavi
Chama cha Wafugaji Mkoa wa Katavi CCWT wameilalamikia Serikali ya Mkoa wa Katavi kwa kushindwa hadi sasa kutenga maeneo ya kuchungia mifugo kama ambavyo alivyoagiza Makamu wa Rais Samia Suluu Hassani kufanya hivyo kwa Mikoa yote hapa Nchini.
Hayo yalisemwa hapo jana na Mwenyekiti wa chama cha wafugaji CCWT Mkoa wa Katavi Mussa Kabushi mbele ya Katibu Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wafugaji Tanzania Magembe Nkonosenema wakati kikao cha wafugaji wa Mkoa wa Katavi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Idara ya Maji na kuhudhuliwa na viongozi wa Halmahauri ya Wilaya ya Mpanda .
Aliema Serikali imeisha towa agizo la kutengwa kwa maeneo kwa ajiri ya kulishia mifugo lakini mpaka sasa wafugaji wa Mkoa wa Katavi hawaja tengewa maeneo hayo na matokeo yake wafugaji wamekuwa wakikamatiwa mifugo yao na kutozwa faini tena bila kupewa risiti za malipo wanayotozwa.
Hivyo chama cha wafugaji kinaiomba Serikali iharakishe kutenga maeneo ya malisho kama walivyo agizwa na Makamu wa Rais Samia Suluu Hassan ilikuepusha migogoro kati ya wakulima, na wafugaji na Serikali .
Kabushi alieleza chama cha wafugaji kimebaini endapo yatatengwa maeneo ya malisho, na mifugo kukaa sehemu moja katika mashamba rasmi wataondoa kero za uharibifu wa mazingira na mwingiliano na sekta zingine kwani kwa takwimu walizo nazo mpaka sasa Mkoa una Ng-ombe 695,433.
Chama cha wafugaji kimekubaliana na wafugaji wote wa Mkoa huu kwa pamoja maeneo yote yatakayotengwa kwa ajili ya malisho watakuwa wanachangia na kulipia kwa kila kichwa Ng-mbe Tsh 5,000 ambapo Tsh 2,000 zitakwenda kwenye kwenye Halmashauri husika na Tsh 3,000 zitakwenda kwenye mfuko wa chama cha wafugaji kwa ajiri ya kuendeleza na kulitunza eneo watakalo tengewa wafugaji .
Nae Katibu wa CCWT Mkoa wa Katavi Mahela Mayanda alisema wafugaji wamekuwa wakikamatwa na Askari wa Hifadhi pamoja na maliasili na wamekuwa wakiteswa vikali ikiwa pamoja na kutozwa faini za juu zinazofikia milioni 15 hadi milioni 20 na kutokuwa linganifu na idadi ya Ngmbe wanazizikamata na kunyimwa stakabadhi ya faini hizo .
Alizungumza kwa masikitiko makubwa alisema zaidi ya Ng-0mbe 5,840 wameuwawa kwa kupigwa risasi katika kipini cha mwaka 2013 hadi 2015 kutokana na kuwa ndani ya eneo la Rukwa Lwafi lililotengwa kama eneo la pori la akiba .
Katibu mkuu wa chama cha Wafufaji Tanzania Magembe Nkonosenema zipo changamoto nyingi sana zinazo wakabili wafugaji wa Mkoa wa Katavi .
Alisema chama cha wafugaji hakitaki wala hakipendi kuwa na malumbano na Serikali bali wao wanachohitaji ni Serikali kutenga maeneo ya wafugaji kwani shughuli ya ufugaji sekta rasmi na ndio maana Rais alimteuwa waziri anae shughulikia Wizara ya mifugo.
Sanjari na hayo Nkonosenema alisema kumekuwepo na tabia ya uanzihwaji wa mapori ya akiba WMA nanayoanzishwa kiujajanja na wamekuwa wakipewa maeneo hayo Wazungu badala ya wazawa.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Thiodela Kisesa aliwataka wafugaji wafuate sheria na waishi kwenye maeneo yaliotengwa kuishi .
Alisema wapo baadhi ya viongozi wa siasa wamekuwa wamekuwa wakiwalazimisha wafugaji kuishi kwenye maeneo yasiyo sitahili kuishi wafugaji wa mifugo .
Alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya mpanda ipo kwenye utaratibu wa kupanga matumizi ya ardhi katika maeneo yote ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda hari itakayosaidia kupumguza migogoro ya wakulima na wafugaji
No comments:
Post a Comment