Na Walter Mguluchuma
Kataviyetu blog
Watu wawili wakazi wa Mtaa wa wa Mji wa Zamani Manspaa ya Mpanda wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa na Risasi 70 za Bunduki aina ya SAR na SMG wakiwa wamezihifadhi ndani ya Kopo la oil.
Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea walikamatwa hapo juzi majira ya saa kumi na moja na nusu jioni huko katika Mtaa wa Mji wa zamani mjini hapa .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia jeshi la polisi kupata taarifa za kutoka kwa Raia wema kuwa watu hao wanamilki Risasi kinyume cha sheria .
Alisema baada ya Polisi kupata taarifa hizo walianza kufanya uchunguzi na ndipo siku hiyo ya juzi walipofanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na Risasi 70 za bunduki aina ya SAR na SMG wakiwa wamezihifadhi ndani ya nyumba yao zikiwe kwenye kopo la OIL lenye rangi ya kijivu.
Wakati huo huo jeshi la polisi Wilayani Mpanda linawashikilia watu wawili wakazi wa Mji wa zamani kwa tuhuma za kuwakamata wakiwa na Bhangi kete 705 na debe mbili za Bhangi wakiwa wamezififadhi ndani ya nyumba wanayoishi.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao wawili ambao majina yao bado yamehifadhi na jeshi hilo walikamatwa hapo juzi majira ya saa kumi na mbili jioni huko katika Mtaa wa Mji wa zamani .
Alieleza mbele ya waandishi wa Habari kuwa watuhumiwa walikuwa wameihifadhi Bhangi hiyo ndani ya mifuko ya sandarusi huku wakiwa wameificha ndani ya nyumba yao wanayoishi .
Kaimu Kamanda Nyanda alisema watuhumiwa wa matukio hayo yote mawili bado wanashikiliwa na jeshi la Polisi na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi wa matukio haya utakapo kuwa umekamilika ili wakajibu Washita Mahakamani yanayowabili .
0 comments:
Post a Comment