Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima amewapiga marufuku wenyeviti wa Mitaa kujihusisha na shughuli ya kukusanya usafi wa mazingira kwani jukumu hilo ni la maafisa watendaji wa Mtaa.
Mwamlima alitowa agizo hilo hapo jana wakati wa kikao cha kamati ya mashauliano ya Wilaya ya Mpanda (DDC kIlichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji mjini hapa.
Alisema kumekuwa na tabia baadhi ya wenyeviti wa mitaa kufanya shughuli ya kukusanya fedha za usafi wakati jukumu hilo ni la watendaji wa mitaa.
Alieleza wenyeviti wa mitaa wao ni watu wakuchaguliwa hivyo kunauwezekano mkubwa kwa wao kushindwa kuwakamata na kuwachukulia hatua watu ambao wanaokuwa wameshindwa kulipa fedha kwa ajiri ya usafi wa mazingira kwa kuwa waliwachagua kwa kuwapigia kura wakati wa uchaguzi.
Hivi karibuni DC huyo alifanya ziara katika Kata ya makanyagio na
kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliowalalamikia wenyeviti wao
kufanya shughuli za kukusanya fedha za usafi wa mazingira wakati
watendaji wa mitaa wapo.
Nae Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda
Gervansi Nyaisonga aliwaeleza wajumbe wakikao hicho kuwa pamoja na
kuwepo na mpango wa elimu bure bado kunatatizo la kundi kubwa la watoto wasio soma shule kutokana na miundo mbinu.
Pia alishauli jina la Wilaya ya Tanganyika
iliyotangazwa kuanzishwa hivi karibuni ni budi likabadilishwa na kuitwa
jina la Wilaya ya ziwa Tanganyika kwani Tanganyika ilikuwa ni jina la
nchi leo hii litumike kama jina la wilaya halitaleta maana nzuri.
Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo aliomba manispaa ya Mpanda wakabidhiwe Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo imejengwa kwenye Manispaa na inawahudumia zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Manispaa hiyo.
Na pamoja kuwa inawahudumia wakazi hao pia wamekuwa wakikosa nguvu za kushughulikia malalamiko ya wananchi wanaopata huduma kwenye hospitali hiyo kwa kuwa hawana mamlaka nayo .
Manispaa ya Mpanda inatumia kituo chake cha afya
cha Mwangaza kama ndio hospitali yake ya manispaa na hawatowi huduma ya
kulaza wagonjwa wanalazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo
ipo katikati ya manispaa ya Mpanda.
0 comments:
Post a Comment