Home » » MTOTO AUWAWA KWA KUPIGWA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUKATAA KUMFULIA NGUO

MTOTO AUWAWA KWA KUPIGWA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUKATAA KUMFULIA NGUO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mtoto  aliyejulikana kwa Jina la   Nchimbi  Tungu(11)  Mkazi wa Kata ya Usevya Wilaya ya Mlele ameuwawa kikatili  na  Mama yake mzazi   Sado Roketi (26) Mkazi wa Kata hiyo  kwa kumpiga na fimbo  katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha  kumning’iza juu ya mti wa mwembe  baada ya kumfunga kamba shingoni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hilo na mama kuuwa mtoto wake wa kumzaa lilitokea hapo juzi  mida ya saa sita mchana kijijini hapo .
 Siku hiyo ya tukio marehemu alipewa nguo na mama yake ili aweze kumfulia  hata hivyo mtoto huyo hakuweza kufua nguo za mama yake kwa kile alichodai kuwa alikuwa amechoka .
Kamanda Kidavashari alisema  ndipo  mama wa marehemu  alipokasirika na kuchukua fimbo  na  kuanza kumpiga  kwa kushambulia  sehemu mbalimbali za mwili wake  huko mtoto huyo akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada na akimsihi mama yake amwachie.
Pamoja na marehemu kuomba  msamaha kwa mama yake hakujari ombi la kuombwa msamaha na aliendelea kumpiga kwa kutumia fimbo   licha ya marehemu kuendelea kulia.
 Kamanda Kidavashari alieleza baada ya kugundua  mtoto huyo amefariki Dunia kutokana na kichapo alichompa    Sodo Roketi  alimchukua mtoto marehemu huyo na kwenda nae kwenye mti wa mwembe na kisha alimfunga kamba na  kumning’iza juu ya mti wa mwembe kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Baada ya  kuwa amemtundika juu ya mti  aliendelea kufanya shughuli zake kama kawaida kwa  ili watu wasimtilie shaka kuhusiana na mauwaji hayo .
Kidavashari alisema Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa  Sado  Roketi na anaendelea kuhojiwa  na mara upelelezi utakapo kamilika  anatarajiwa kufikishwa Mahakamani ili aweze kujibu tuhuma   zinazomkabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa