Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mtafaharuku
mkubwa juzi umetokea
juzi katika shirika
la Hifadhi la chakula cha akiba
la Taifa ( NFRA) tawi la Mpanda
Mkoa wa Katavi baada ya shirika
hilo kusitisha huduma ya
utoaji wa mahindi kwa wafanyabiashara wenye vibali
vya kusafirisha mahindi kutoka kwenye tawi la Mpanda kupeleka Mikoa ya Tabora Simiyu ,Geita na Musoma
Tukio hilo
lilitokea hapo juzi baada ya Meneja wa
NFRA wa Tawi la Mpanda
Richald Ruah kuwa somea
barua wafanya biashara hao wenye
vibali vya kununua mahindi kwenye tawi la Mpanda na badala yake waende wakanunue kwenye matawi ya Laile na
Sumbawanga Mkoani Rukwa barua yenye kumb
\ na \ Fa154\ 201\ 01 iliyosainiwa
na Anna
Ngoo kwa niaba ya Afisa mtendaji
wa Mkuu wa NRFA.
Wafanyabiashara
hao baada ya kusomewa barua hiyo wote
kwa pamoja walipinga kitendo cha shirika hilo
la kuwataka wakachue mahindi Mkoani Rukwa badala ya Tawi la Mpanda
na ndipo walipoanza kutowa kauli za
kupiga uamuzi huo .
Mmoja wa
wafanyabiashara hao Peter Masanja
alieleza kuwa yeye alipewa kibali
cha kununua mahindi kutoka tawi la Mpanda kupeleka Kanda ya ziwa kwenye Mikoa yenye
njaa hivyo hayuko tayari kwenda
kuchukulia mahindi yake Sumbawanga kwani kibali chake kinamruhusu kununulia mahindi yake Mpanda
Katavi .
Costantino Cosmas
mfanyabiashara kutoka Kaliuwa Mkoa wa Tabora alisema kitendo NFRA
kuwasitishia vibali vyao vya kuchukulia mahindi Mpanda watakuwa wamepata hasara
kubwa hivyo hayuko tayari kutekeleza agizo la barua hiyo.
Alisema yeye
alikuwa ameisha anza kupatia mahindi yake kwenye behewa la treni katika sitesheni ya Mpanda na
tayari alikuwa amefikisha nusu ya behewa na hawezi
kwenda kufuatia mahindi ya kujazia bahewa lake
kwa kuogopa kulipia chaji ya
kuchelewesha kupakia mzigo kwenye behewa.
Frolensi Malwa ambae ni mfanyabiashara wa kutoka
Musoma alieleza kuwa yeye ameisha lipia kwenya Tawi hilo la Mpanda tani 185 za mahindi kwa bei ya tsh 380 kwa kilogramu moja .
Alisema na wenye
maroli ya kusombea mzigo wake huo
ameisha walipa kupakia mzigo kuanzia
Mpanda kwenda Musoma na sio Sumbawanga au Laile
na gharama ya kusafirishia mzigo tofauti na tawi la Mpanda hana uwezo nao kwani fedha za kununulia
mahindi hayo alikopa Benki ipo hatari kwake
hata ya kushindwa kurejesha mkopo huo.
Nae Maneno
Masanja alisema hayuko
tayari kufuata agizo la barua hiyo kwani amekaa zaidi ya wiki mbili akisubilia foleni ya kupakia mahindi na mpaka
sasa ameisha ishiwa hela na alikuwa
anakunywa bia sasa hivi hata uwezo wa kunywa bia hana analazimika kunywa viroba.
Alieleza
kuwa NRFA walipaswa kutowa taarifa ya kusitisha vibali hivyo mapema sio kama walivyowafanyizia juzi ni kitendo kibaya kwa wafanyabiashara hao .
Nae Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ambae alifika kwenye eneo hilo kuwasikiliza
wafanya biashara hao huku akiwa na ulinzi Mkali
wa Askri Polisi waliokuwa na
mabomu ya machozi na silaha za moto kutokana na hari iliyokuwepo hapo .
Mwamlima
aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa NRFA imekubali kuendelea kuwazia wafanya biashara hao mazao ya mahindi
kwenye tawi la Mpanda kama ambavyo vibali vyao vinanavyoeleza mpaka hapo
vitakapo kwisha hari ambayo iliwafanya
wafabiashara hao waanze kushangilia.
Pia alishauri
kuwa ni vizuri taarifa zinazohusu
mabadiliko yanayofanywa na NRFA taarifa zake ziwe zinatolewa mapema
kuliko taarifa za kushitukizwa kama ilivyotokea juzi.
No comments:
Post a Comment