Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imewahukumu watu wawili
Stephano Jonas (22) na Franko Hamisi( 18) Wakazi
wa Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi
wamehukumiwa jumla ya kifungo cha miaka 40 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 27
Hukumu hiyo
ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odira Amwol baada ya Mahakama kulidhika na ushahidi
uliotolewa mbele yake na upande wa mashitaka .
Awali katika kesi
hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria wa
Serikali Jamila Mziray alidai Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao
kwa pamoja walikamatwa hapo mei 15 mwaka
huu majira ya saa tisa usiku wakiwa
katika Kijiji cha Mnyaki Makazi ya Wakimbizi ya Katumba.
Mziray alieleza
kuwa watuhumiwa hao walikamatwa
kufuatia taarifa walizokuwa wamezipata Askari wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) wa
mbuga ya Katavi na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.
Alieleza baada ya
kuwa wamepata taarifa hizo Askari hao
walikwenda kwenye Kijiji cha Mnyaki na
walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na meno ya Tembo vipande vitatu vyenye uzito wa kilogramu
nane yenye thamani ya shilingi milioni 27,760,000 wakiwa wameyahifadhi
chini ya kitanda katika nyumba ya
Jackisoni Elasto ambae alikuwa ni
mshitakiwa wa taatu.
Washitakiwa hao
katika utetezi wao walidai kuwa meno
hayo ya Tembo hayakuwa yao bali yalikuwa
ni ya Jackisoni Elasto
ambae kwenye kesi hiyo alikuwa ni mshitakiwa wa tatu na alikuwa amewatuma
wapeleke Daress salaam kwa mtu mmoja
anae julikana kwa jina la Alex na
wayasafirishe meno hayo kwa njia ya
Treni.
Hakimu Amwol baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa
kesi hiyo na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na
mashidi saba na washitakiwa walijitetea wenyewe aliieleza Mahakama kuwa pasipo chaka
yoyote Mahakama imelidhika na ushahidi
wa upande wa mashitaka na
watuhumiwa wawili wamepatikana na hatia.
Hivyo aliwapa nafasi watuhumiwa ya kujitete kama watakuwa na sababu ya msingi
ya kuishawishi mahakama iwapunguzie adhabu .
Mshitakiwa wa
kwanza Stephano Jonas
aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa mama yake mzazi na wadogo
zake watatu wanamtegemea yeye .
Nae mshitakiwa wa
pili Franko Hamisi aliomba Mahakama
impunguzie adhabu kwa kuwa anaumri mdogo
wa miaka 18 na mama yake mzazi anamtegemea yeye na pia hana baba kwani baba
yake alishafariki Dunia.
Mwanasheria wa
Serikali Jamila Mziray baada ya utetezi huo aliupinga vikali na aliiomba Mahakama
itowa adhabu kulingana makosa ya vifungu vya sheria walivyopatikananavyo ili iwe fundisho pia kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Hakimu Odira
Amwol baada ya kusikiliza ombi la washitakiwa
la kuomba kupunguziwa adhabu alisoma hukumu kwa kueleza
kuwa Mahakama imewatia hatiani washitakiwa Stephano Jonas na Franko Hamisi na Mahakama imewakumu
kutumikia kila mmoja kifungo cha miaka
20 jela .
Mahakama hiyo
ilimwachia huru mshitakiwa watatu Jackisoni Elasto baada ya kukosekana kwa
ushadi wa kumtia hatiani uliotolewa na
upande wa mashitaka .
Hivi karibuni
Mahakama hiyo iliwahukumu watu wawili kutumikia jela kifungo miaka 42 baada ya kupatikana na kosa
la kukamatwa na meno ya Tembo ya thamani ya milioni 60.
No comments:
Post a Comment