Tuesday, December 22, 2015

WASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KUMPIGA MWANAMKE WANAE MTUHUMU MCHAWI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia watu  wawili kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga na kumjeruhi  Jeneroza  Roba (60) Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Mjini  Mpanda baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa  tukio la kupigwa na kushambuliwa kwa mwamke huyo lilitokea hapo juzi majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa Mji wa Zamani mjini hapo.
Kidavashari aliwataja  waliokamatwa na Polisi kuwa ni  Ashura  Msaguzi (30) Mkazi wa Mji wa Zamani ambae ni mtumishi wa chuo cha maendeleo ya jamii cha Msaginya Mkoani hapa na  Aisha Sungura (28) Mkazi wa mtaa wa mji wa Zamani.
 Alisema siku hiyo  ya tukioj Jeneroza alikuwa akipita kwenye mtaa wa mji  wa Zamani akiwa anaelekea nyumbani kwake  katika Mtaa wa Nsemlwa
Ndipo   mtuhumiwa Ashura  alipomwona Jeneroza  na kuanza  kupandisha mashetani huku akiwa anamtaja  Jeneroza kuwa ndie aliyemloga .
Kitendo hicho cha kupandisha mashetani  kilimshawishi  Aisha  kuungangana na  Ashura na kisha  walianza kumshambulia  kwa kumpiga Jeneroza  na  kisha walimvua nguo na kumwingiza ndani ya nyumba hiyo
Alisema  kitendo hicho kiliwakasirisha watu walioshudia  hari ambayo iliwafanya wananchi waanze kuishambulia kwa mawe nyumba hiyo kwa lengo la kumwokoa Jeneroza ambae alikuwa amefungiwa ndani ya  nyumba ya wazazi wake na Ashura.
Kidavashari alieleza Mwenyekiti wa Mtaa huo  Magreti John(Mhaya) alifika kwenye eneo hilo na baada ya kuona  hari ya  wananchi ya kuishambulia  nyumba hiyo kwa mawe ikiwa inazidi kuongezeka alitowa taarifa kwa jeshi la Polisi  .
Polisi baada ya kufika kwenye eneo hilo waliweza kuwatawanya wananchi hao na  waliweza kufanikiwa kumtowaNdani ya nyumba Jenaroza na  kuwakamata watuhumiwa na  kuwafikisha katika kituo cha Polisi cha Mpanda .
Kamanda Kidavashari alisema watuhuwa bado wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na mara upelelezi utakapo kamilika  wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani  ili wakaji mashika yanayo wakabili.
Amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikoni  pindi panapo kuwa pametokea migogoro ya  ya maswala ya kijamii na badala yake waende kwenye vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment