Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Kazimili (49)
Mkazi wa Kitongoji cha Misenga Tarafa ya Mwese ameuwawa kikatili kwa kukatwa katwa na shoka na mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake wakati akiwa
amelala chumbani kwake na mke wake.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa tukio la mauwaji hayo ya
kikatili lilitokea hapo juzi majira ya
saa saba usiku nyumbani kwa marehemu huyo .
Alisema siku hiyo
ya tukio marehemu alikuwa amelala kwenye nyumba yake ndani ya chumba chake akiwa na mke wake waliyekuwa
wakiishi nae pamoja na watoto wake .
Kidavashari
alieleza wakati marehemu akiwa amelala ndani
watu wasiofahamika walifika nyumbani kwake na kuvunja mlango wa mbele wa
nyumba yake hiyo huku wakiwa na silaha
aina ya shoka na mapanga.
Baada ya kuwa wamevunja mlango wa mbele watu
hao waliingia ndani hadi mahali alipokuwa amelala marehemu na mkewe na kisha walimtowa sebuleni marehemu huku wakiwa wamemlazimisha
mkewe asitoke nje wala asipige kelele.
Kidavashari
alieleza baada ya kuwa wamemtowa sebuleni walianza kumshambulia kwa kumkatakata
kwa silaha za panga na shoka katika seheme mbalimbali
za mwili wake za kichwani
shingoni na kwenye mikono yake huku marehemu huyo akiwa anapiga mayowe ya
kuomba msaada kwa majirani zake.
Alisema pamoja na marehemu kupiga mayowe wauwaji hao hawaku jali na waliendelea
kumkatakata marehemu hadi walipoona amefariki dunia ndipo walipotokomea kusiko julikana.
Majirani walifika
kwenye eneo hilo na walikuta mwili wa
marehemu ukiwa umegalagala chini huku ukiwa umekatwa katwa katika sehemu
mbalimbali za mwili wake.
Kamanda
Kidavashari alisema mpaka chanzo cha
kifo hicho cha mauwaji ya kikatili hakijafahamika na jeshi la pollsi wa kushirikiana na
wananchi wa Kitongoji hicho wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu
waliohusika na mauwaji hayo.
0 comments:
Post a Comment