Home » » AKAMATWA AKIWA ANAICHI NCHINI BILA KIBALI AKIWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA

AKAMATWA AKIWA ANAICHI NCHINI BILA KIBALI AKIWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi linamshikilia  Raia wa Nchi ya Burundi  aliyefahamika kwa jina la Michael  Lubandaya (18) Mkazi wa Nyanza   Nchini   Burundi huku akiwa anaishi  nchini  bila kibali
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa  Katavi  Dhahiri Kidavashari   aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo  juzi  majira ya  sita na nusu  mchana huko katika Kijiji cha  Kibaoni  Wilaya ya Mlele  Mkoani  Katavi
 Alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa kufuatia  taarifa za raia wema  walizozitowa kwa jeshi la Polisi baada ya kumtilia mashaka juu ya uraia wake
 Kidavashari alieleza baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la Polisi walifanya msako wa kumsaka mtuhumiwa  huyo   na ndipo siku hiyo  walipofanikiwa kumkamata
Baada ya kufanyiwa mahojiano ya kina na polisi mtuhumiwa  Michael  Lubandaya  aligundulika  kuwa   amejihandikisha  huko  Kakese  Manspaa ya Mji wa Mpanda  katika  daftari  la kudumu  la wapiga  kura  kwa jina la  Abdallah  Yusuph
Na  alipatiwa  kitambulisho  cha wapiga kura  kilichotolewa na Tume ya uchaguzi ya Taifa  chenye  namba  t-1000-756-1
Kidavashari  alisema  katika uchunguzi wa awali mtuhumiwa  alibainika  kuwa sio  rai wa Tanzania  ni Raia wa Burundi  na alijiandikisha kwenye  daftari la kudumu la wapiga kura huku  akitambua kufanya hivyo  si  halali  kufanya hivyo
 Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi  utakapo kuwa umekamilika ili  ajibu mashitaka  ambayo yanamkabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa