Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na askari
wa Hifadhi ya Taifa ya wanyama poli ya
Katavi(TANAPA) wamefanikiwa kukamata bunduki moja
aina ya SMG ikiwa na
magazine mbili na Risasi
110 za SMG zikiwa
zimefishwa katika Kijiji cha Nzaga
kata ya Ulwira Wilaya ya
Mlele Mkoa wa Katavi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia jana waandishi wa
Habari kuwa Askari hao walikamata silaha hiyo hapo jana
majira ya saa nane usiku
kijijini cha Ulwira
Alisema kabla ya tukio Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na
polisi walipata taarifa
kutoka kwa raia wema kuwa
kuna mtuhumiwa mmoja
jina limehifadhiwa mtuhumiwa
huyo ambae ametoroka kwa kuwa
bado anatafutwa kuwa anajishughulisha na shughuli
za ujangili na anamiliki
silaha moja ambayo
inaitumia kwa shughuli hizo na ameifisha
shambani kwake
Hivyo baada ya taarifa hizo kuwa zimepatikana jeshi la
polisi kwa kushirikiana na TANAPA
walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa kwa lengo la kufuatilia tuhuma hizo
Kamanda Kidavashari alisema baada ya Askari hao kufika nyumbani kwa
mtuhimwa waliizingira nyumba yake
na ndipo walipoingia ndani ya nyumba yake aliyokuwa akiishi na familia
yake walikuta ameisha toroka
Alieleza
Askari hao walifanya upekuzi na walifanikiwa kukamata bunduki moja aina ya SMG
yenye namba C 2136 ikiwa na magazine mbili pamoja na
risasi 110 za SMG zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa salphet akiwa amezichimbia chini ya ardhi
katika eneo la nyumba yake
Kamanda
Kidavashari alisema pamoja na mtuhumiwa huyo kuwa ametoroka juhudi
za kumtafuta zinaendelea pamoja
na kuwasaka washirika wanzake
ambao amekuwa akishilikiana nao kufanya
ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba
0 comments:
Post a Comment