Friday, April 24, 2015

WAKAMATWA NA BUNDUKI TATU AINA YA GOBOLE NA RISASI 16 PASIPOKUWA NA KIBALI CHOCHOTE.


watu watano wakamatwa na bunduki aina ya Gobole na Risasi
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu  watano wakazi wa Kata ya Ugala Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi    kwa tuhuma    za  kuwakamata katika matukio matano  tofauti  wakiwa wanamiliki  Bunduki tatu aina ya Gobole na Risasi kumi na sita bila kuwa na kibali
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kuwa watuhumiwa hao wote watano  walikamatwa  katika  mida  tofauti hapo juzi wakiwa katika Kijiji cha Ugala   Tarafa ya Ndurumo Wilaya ya Mlele
 Tukio la kwanza lilitokea  majira ya saa  kumi  jioni ambapo mtu aliyefahamika kwa jina  la  Lazaro  Zakaria (63) Mkazi wa Kijiji hicho alikamatwa  akiwa  na Bunduki aina ya  Gobole  lenye Namba za usajiri  NZ 600 ambayo alikuwa  akiimiliki bila kuwa na kibali
 Tukio la Pili  lilitokea hapo majira ya saa  kumi na mbili jioni  mtu mmoja alitambulika kwa jina la  Robarti Kaumba (80)  mkazi wa Kijiji  cha ugala alikamatwa akiwa nyumbani kwake  na Bunduki moja aina ya Gobole  isiyokuwa na  namba na alikuwa akiimiliki kinyume cha  sheria
 Kidavashari  aliendelea kuwaeleza waandishi wa Habari kuwa tukio la tatu lilitokea siku hiyo hiyo ya  juzi majira ya saa moja usiku ambapo  mtu aliyefahamika kwa jina la  Shabani Mussa (52)  Mkazi wa Kijiji  cha  Katombola  Kata ya Ugala  alikamatwa akiwa na Bunduki aina ya Gobole aliyokuwa akiimiliki bila kuwa na kibali
 Alisema katika tukio jingine  Benedictor  Simon(52) Mkazi wa Kijiji cha Ugala alikamatwa akiwa nyumbani kwake  majira ya saa tano usiku huku akiwa na Bunduki aina ya Gobole  na  Risasi 15 ,vipande tisa za nondo  vipande vya mti wa  mtutu wa bunduki  na Baruti aliyokuwa amehifadhi ndani ya chupa
 Na  katika tukio jingine lililo tokea siku hiyo  majira ya saa saaba usiku   Shabani Mussa (52) Mkazi wa Kijiji cha  Ugala  alikamatwa akiwa  na  Risasi moja ya Gobole akiwa anamiliki bila kibali
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kufutia msako uliofanywa na Askari wa Jeshi la Polisi na TANAPA
 watuhumiwa hao  wanaendelea kushikiliwa na Polisi  na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika
    
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

No comments:

Post a Comment