Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mamlaka ya dawa na chakula (TFDA) Kanda ya Nyanda za juu kusini imeteketeza kwa kuchoma moto dawa za binadamu ambazo zimepigwa marufu Vipodozi na bidhaa za chakula ambazo hazina ubora na hazifai kwa matumizi ya binadamu zenye thamani ya zaidi ya milioni tano walizozikamata kufutia msako walioufanya katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Mkaguzi wa Kanda ya nyanda za juu kusini wa (TFDA) Paulo Sonda aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kuwa dawa hizo walizoziteketeza kwa moto pamoja na bidhaa za chakula na vipodozi walizoziteketeza walifanikiwa kuzikamata katika msako walioufanya kwa siku tatu katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Alisema katika msako huo walioufanya kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya wa Halmashauri za Wilaya ya Mpanda waliweza kubaini bidhaa zilizopigwa marufuku zikiwa zinauzwa kwenye maduka mbalimbali
Sonda alizitaja baadhi ya dawa na bidhaa walizozikamata na kuzitekekeza kuwa ni Amodiaquine, Paracetamol vipodozi vyenye viambata vya mecury
Nyingine alizitaja kuwa ni bidhaa za Juice , Biscut na Kahawa ya kutoka Nchi ya Burundi ambazo hazina ubora ambazo waliziingiza nchini kwa njia ya panya thamani ya dawa vipodozi na bidhaa hizo walizoziteketeza zilikuwa na thamani ya milioni tano na laki tisa
Alisema dawa hizo na bidhaa zisizokuwa na ubora zimekuwa na athari kubwa kwa watumiaji hivyo wafanya biashara wanaowajibu wa kuhakikisha bidhaa wanazoingiza nchini na kuziuza wawe wanazihakikisha zinakuwa na ubora unaokubalika
Alifafanua kuwa watumiaji wa dawa na bidhaa kabla ya kununua mahitaji yao wawe na utaratibu wa kuzikagua kwa kuangalia alama zinazokuwa zimewekwa kama zinazoonyesha ubora wa bidhaa
Alitaja changamoto wanayokabiliana nayo TFDA ni tabia inayofanywa na wafanya biashara kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa kupitia mipaka isiyo rasmi (njia za panya)
Nae Mfamasia wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Victor Kabanga alieleza kuwa katika kukabiliana na hari hiyo tayari kuna timu ya wataalamu katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda inafanya kazi ya kuhakikisha dawa na bidhaa ambazo hazina ubora haziingii katika Mji wa Mpanda
Alisema zoezi hilo ni endelevu hivyo wafanya biashara wasifikirie kuwa msako huo ulikuwa ni wa muda bali ni zoezi endelevu litakalo kuwa linafanyika wakati wote
Kabanga alieleza pia wataendelea kutowa elimu kwa wafanya biashara juu ya athari yaa kuingiza bidhaa na kuwauzia wananchi bidhaa ambazo hazina ubora unaokubalika
Alifafanua kuwa TFDA imeisha towa mamlaka kwa Halmashauri kutumia wataalamu wake wa afya kufanya ukaguzi wa kubaini dawa za binadamu vipodozi na bidhaa za chakula ambazo wafanyabiashara wanaziuza ambazo hazisitahili kuuzwa
Zoezi hilo la kuteketeza bidhaa hizo zilifanyika katika dampo lililoko katika eneo la Minsumilo na kushuhudiwa na wataalamu kutoka TFDA Kanda ya nyanda za juu kusini na wataalamu wa Afya kutoka Halmashauri za Mji wa Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali
No comments:
Post a Comment