N a Walter
Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mtu mmoja Mkazi
wa Kata ya Ugala Tarafa ya Ndurumo Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kwa tuhuma za kumkamata akiwa na mtambo wa
kutengenea silaha Bunduki aina ya Gobole
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi
Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa mtuhumiwa
huyo aliyekamatwa kuwa ni
Hamisi Rehani (68) Mkazi wa Kata ya Ugala Wilaya ya Mlele
Mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo jana majira ya
saa kumi na mbili jioni wakati akiwa
ameuhifadhi mtambo huo wa kutengenezea Bunduki aina ya Gobole ndani ya nyumba yake aliyokuwa akiishi yeye na familia yake
Kidavashari alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia
taarifa zilizokuwa zimetolewa na raia
wema kwa jeshi la polisi kuwa mtuhumiwa Hamisi Rehani amekuwa akijihusisha na utengenezaji wa bunduki aina ya Gobole bila kuwa na kibali
Alifafanua baada ya taarifa hizo kulifikia
jeshi la Polisi lilikwenda kwenye Kata hiyo ya Ugala wakiwa wamefuatana
na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Kidavashari alieleza baada ya Askari hao kuwa
wamefika nyumbani kwa mtuhumiwa waliweza kumpekuwa ndani ya nyumba yake na
ndipo walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa
akiwa na mtambo wa kutengenezea Bunduki aina ya Gobole
Alisema uchunguzi wa awali uliofanywa na
Askari wa Polisi na Askari wa TANAPA unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mtambo huo
kwa ajiri ya kuwatengenezea Bunduki aina
ya Gobole wawindaji haramu ambao
wamekuwa wakiwinda wanyama kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Mtuhumiwa Hamisi Rehani anatarajiwa kufikishwa
Mahakamani mara baada ya uchunguzi wa tukio hilo utakapo kuwa umekamilika ili
aweze kujibu mashita yanayomkabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment