Na
Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la Paulo Luzuba (70) Mkazi wa Kijiji
cha Vikonge Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefariki Dunia wakati akiwa
anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya kupigwa
na watu wasiojulikana
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari marehemu huyo alifariki
Dunia hapo juzi majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Wilaya ya
Mpanda alikokuwa akipatiwa matibabu
Alisema kabla ya
tukio hilo siku ya tarehe 16 machi majira ya saa
nane mchana marehemu aliondoka nyumbani kwake kwa lengo
la kwenda mnadani kununua mahitaji ya nyumbani kwake
akiwa na mjukuu wake aliyejulikana kwa jina
la Wiliamu Shija(20)
Alifafanua
walipofika kwenye eneo la mnada marehemu alinunua mahitaji yake ya
nyumbani chumvi,sabuni na dagaa na kisha alimpatia mjukuu wake apeleke
nyumbani na yeye alibaki kwenye eneo hilo la mnada
Kidavashari
alisema siku hiyo marehemu hakurejea tena nyumbani mpaka siku
iliyofuata ya tarehe 17 machi majira ya saa nne asubuhi
ambapo marehemu alionekana karibu na eneo la mnadani huku akiwa na
majeraha usoni na kichwani na huku akiwa uchi na akiwa
amepoza fahamu
Marehemu
alichukiliwa na ndugu zake na kupelekwa Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya maatibabu ambapo juzi
alifariki Dunia wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu
Kamanda
Kidavashari alieleza mpaka sasa chanzo cha
mauwaji hayo bado haijajulikana na hakuna mtu wala watu
waliokamatwa kuhusiana na mauwaji hayo na Jeshi la polisi kwa
kushilikiana na uongozi wa Kijiji linafanya upelelezi ili
kubaini na kuwakamata watu wote waliohusika katika mauwaji ya
Mzee huyo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment