Home » » HATARI: MWANAFUNZI AUWAWA KWA KUPIGWA NA BABA YAKE MZAZI

HATARI: MWANAFUNZI AUWAWA KWA KUPIGWA NA BABA YAKE MZAZI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwanafunzi  aliyefahamika kwa  jina la Alson  Kibona (17) mwanafunzi wa  kidato cha nne  shule ya Sekondari  Nsemlwa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  ameuwawa baada ya kupigwa       kichwani na  mpini wa  koleo na nasehemu mbalimbaliza mwili wake   na  baba yake  mzazi  kwa kosa la kutokwenda shuleni
Kaimu  kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi   Rahid  Mohamed  alimtaja  mzazi  anayetuhumiwa  kumuuwa  mwanae  kwa kumpiga na mpini wa koleo kuwa ni  John Kibona(35)  mkazi wa  mtaa wa Nsemlwa  Mjini  hapa
 Alisema tukio hilo  hilo la mauwaji ya mwanafunzi  lilitokea hapo juzi majira ya saa tisa usiku  nyumbani  kwa mtuhumiwa  katika mtaa wa Nsemlwa
 Kwa  mujibu wa  Rashid  Mohamed  Siku  hiyo ya tukio   marehemu  Alson alikuwa amelala  chumbani   mwake ndipo  baba yake  alipomwamusha na kuanza kumuoji  kwanini amekuwa na tabia ya utoro  wa mara kwa mara wa kutokwenda shuleni
Mohamed  alisema   ndipo mtuhumiwa  alianza  kumpiga marehemu  kwa kutumia  mpini wa koleo kichwani na sehemu mbalimbali za  mwili wake  huku akiwa akimkanya kwa maneno kuwa  aache tabia ya utoro wa shuleni
 Alisema marehemu baada ya  kuona kupigo kimemzidia  alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada  hata hivyo mtuhumiwa hakujali aliendelea  kwa  kumpa kichapo  mwanae huyo
 Siku iliyofuata marehemu aliaka  huku  akiwa na maumivu makali katika sehemu mbalimbali za mwili wake hari ambayo ilimlazimu ashindwe hata kwenda shule  na mthumiwa hakujali  wala kumpeleka kwenye matibabu
 Kaimu   Kamanda  Rashid  Mohamed  alieleza  siku  hiyo ilipotimia majira ya saa  sita marehemu  alikwenda kisimani kuteka maji ya kuoga  ambapo alipoinama iliachote maji  damu  zilianza kumtoka  mdomoni  na puani  na kisha kuanguka  chini pembezoni mwa kisima hicho
 Alisema  majirani waliokuwa karibu na eneo hilo walimchukua  marehemu  na kumpeleka  katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  kwa ajiri ya kupatiwa matibabu
Alifafanua wakati  akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo  alifariki Dunia  kutokana na  majeraha makubwa  aliyokuwa ameyapata  kutokana  na kipigo  alichokuwa amekuwa amekipata
 Baada  ya mthumiwa  kupata taarifa  kuwa mwanae  amepelekwa Hospitali  na wakati akiwa anapatiwa   matibabu amefariki Dunia  aliamua  kutoweka  na kukimbilia  sehemu   kusiko julikana
 Kaimu  Kamanda  wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  alisema jeshi la polisi  kwa kushirikiana  na ndugu wa  marehemu  na uongozi wa mtaa  linamsaka  mtuhumiwa  ili  kumkamata  na aweze  kujibu tuhuma  inayomkabili
 Aidha kaimu  kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi  ametowa wito  kwa wazazi na walezi  kuacha  tabia  ya kutumia   nguvu  kwa kuwapiga watoto wao  na badala yake  wawaelimishe  na kuwaeleza  umuhimu  wa elimu  ili  kuepuka  matukio mbaya  ya nanma hii ndani ya jamii
MWISHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa