Home » » RC AMWAGIZA DC KUFUATILIA MATUMIZI YA FEDHA ZA UJENZI WA MAJENGO YA MAABARA

RC AMWAGIZA DC KUFUATILIA MATUMIZI YA FEDHA ZA UJENZI WA MAJENGO YA MAABARA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga kupeleka wakaguzi kwenye shule za Sekondari   kufuatilia matumizi ya  fedha zilizotumika kwa ajiri ya ujenzi wa majengo ya maabara  ya shule za sekondari katika Halmashauri ya Nsimbo baada ya kutoridhishwa  na   ubora wa majengo  hayo
Agizo hilo  alilitowa hapo jana wakati alipokuwa akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya maabara  ya shule za sekondari za Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
 Alisema katika majengo  ya maabara aliyotembelea na kukagua  hajaridhishwa na ubora wa majengo hayo hari ambayo inatia shaka  ya matumizi yaliyotumika  ya  fedha  za ujenzi wa maabarahizo
Dr  Msengi alieleza inashangaza sana kuona majengo ya serikali  yanajengwa kwa gharama kubwa  zaidi kulikomajengo ya watu binafsi  na huku yakiwa yamejengwa  chini ya kiwango
 Alisema majengo ya Serikali yamekuwa yakijengwa ovyo kwa kuwa yamekuwa na usimamizi mbovu na matokeo yake yamekuwa yakiharibika hata kabla ya  kuanza kutumiwa  kutokana na kutosimamiwa  ipasavyo kwenye kila hatua yanapokuwa yanajengwa
 Alifafanua majengo ya Serikali yamekuwa yakijengwa chini ya kiwango huku viongozi wa  maeneo husika  wakiwa wanaangalia tuu  kwa ajiri ya kuwaogopa wakandarasi
 Wakati wa  wakandasi kufanya kazi zao kiujanja ujanja umekwisha  wakandarasi wanamna hiyo watafute sehemu nyingine yakufanyia kazi sio Katavi  kwa sasa
 Pia  alisema  kuwa amefuta ziara za Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo ambayo walikuwa wamepanga kuifanya kwenye baadhi hapa nchini  iliwasimamie maabara   kwenye Kata zao hadi zikamilike
 Rc katika zira hiyo alitembelea shule za Sekondari za Kasokola , Kanoge , Mtapemda ,Nsimbo  na Kenswa    zilizopo katika Halmashauri ya Nsimbo na kugundua kasoro  mbalimbali  kwenye majengo hayo
Miongoni mwa kasoro hizo ni  kuta  za majengo kujengwa huku zikiwa   zimepinda  madirisha na milango  kutengenezwa kwa mbao zisizofaa hari ambayo ilimlazimu  mkuu huyo wa Mkoa  kuwaagiza wakandarasi  kufanyia    marekebisho ya kasoro alizozigundua
Pia majengo hayo yenye kasoro  wakandasi wasipewe fedha tena mpaka hapo watakapo kuwa wamerekebisha  na yeye atapita tena  kuyakagua majengo hayo ya maabara
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Kanali  Ngemela Lubinga  alieleza kuwa maagizo hayo yaliotolewa na Mkuu wa Mkoa atayafanyia kazi  mapema iwezekanavyo
 Inashangaza sana  kuona   kila mkuu wa Idara katika  Halmashauri  anadigilii lakini wanashindwa kusimia  vizuri shughuli za Halmshauri tofauti na watu wenye elimu ya kawaida  anatamani sana Wakurugenzi wa Halmashauri  zote hapa Nchini wawe wanajeshi  alisema  Kanali Lubinga

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa