Na Walter Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inategemea kutumia jumla ya shilingi milioni 680,250,000 kwa ajiri ya kufanya matengenezo ya barabara zake zenye urefu wa Kil0meta 73 ambaz0 ni sawa na asilimia 17.7 ya mtanda wa barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Hayo yalielezwa hapo jana kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo na mwenyekiti wa kamati ya uchumi ujenzi na mazingira Diwani Hamad Mapengo
Alisema katika kipindi cha mwezi julai mwaka huu wa 2014 hadi mwezi septemba 2014 Halmashauri hiyo imeendelea kuzifanyia matengenezo barabara mbalimbali za Halmashauri hiyo
Mapengo alizitaja barabara hizo kuwa ni ujenzi wa daraja la mto Itunya upo katika asilimia 50 ya utekelezaji na utekelezaji bado unaendelea na ujenzi wa daraja la mto Kafisha ambao tayari umeisha kamilika
Alifafanua Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda inazobarabara za kiwango cha changalawe zenye urefu wa kil0meta 172 na na barabara za udongo ni kilometa 239.9
Alisema kutokana na barabara hizo kuwa nyingi ni zaudongo wakati wa masika uharibika na hivyo kupelekea usumbufu mkubwa kwa watumiaji
Mapengo alitaja changamoto nyingine kuwa ni bejeti inayotolewa na serikali ni ndogo hivyo haikidhi kuhudumia mitandao ya barabara zilizopo katika Halmashauri ya Mpanda
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni fedha za mfuko wa barabara zinafika kwa kuchelewa na hivyo kupelekea kazi kutokamilika kwa wakati katika mwaka wa fedha uliopangwa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment