Na Walter Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamshikilia mtoto Frenk Stephano (14) Mkazi wa Kijiji cha Itenka Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenzake (3) mkazi wa Kijiji hicho cha Itenka
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo Novemba 18 majira ya saa mbili usiku nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo Kijijini hapo
Alisema siku hiyo ya tukio wazazi wa mtoto huyo aliyebakwa walikuwa nyumbani kwao wakisubilia kula mlo wa usiku ndipo walipo mlio mkali wa risasi za bunduki jirani na nyumba yao
Kidavashari alieleza baada ya kusikia mlio huo wa risasi za bunduki wazazi wa mtoto huyo waliamua kukimbia mbio na kwenda kujifisha kichana huku wakiwa wamemuacha mtoto wao ndani ya nyumba yao
Alifafanua wazazi hao baada ya kukaa muda mrefu huko walikokuwa wamekimbilia kujifisha na kuona hari imekuwa shwari waliamua kurudi nyumbani kwao ilikwenda kujua mtoto wao waliomuacha atakuwa kwenye hari gani
Kidavashari alisema walipofika nyumbani kwao waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mtuhumiwa Frenk Stephano ambae ni jirani yao akiwa chumbani huku akiwa amelala kitandani na mtoto huyo
Alisema hari hiyo iliwashitua sana wazazi wa mtoto huyo na walianza kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani hata hivyo mtuhumiwa huyo aliweza kutoka nje na kukimbia kabla ya majirani kufika kwenye eneo hilo
Alifafanua wazazi wa mtoto huyo walikuta mahari alipokuwa amelala mtoto wao kitandani huku akiwa ametapakaa mbegu za kiume kwenye sehemu zake za siri huku akiwa akilia kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia
Kidavashari alisema jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi kukamilika ili mtuhumiwa Frenk Stephano aweze kujibu tuhuma ya ubakaji inayomkabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment