Na Walter Mguluchuma
Katavi
Baraza la Madiwani wa Halimashauri ya Nsimbo
Mkoani Katavi limeyataka makampuni
ya uchimbaji wa madini yanayokuja
kufanya utafiti na kuchimba madini kwenye
maeneo ya Halimashauri hiyo yawe
yanakwenda kuripoti
kwenye uongozi wa Serikali ya
kijiji husika kabla hawajaanza kufanyashughuli
Baraza la
Madiwani lilitowa kauli hiyo hapo juzi kwenye kikao cha baraza
la madiwani wa Halimashauri hiyo
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halimashauri ya Nsimbo
Diwani wa Kata
wa Kata ya Magamba Philipo
Kalyalya alikuwa ndio
mchangiaji wa kwanza kutowa
malalamiko kwenye Baraza hilo kuhusiana
na makampuni ya uchimbaji wa madini
Alisema imekuwa ni tabia ya makampuni yanayofanya
utafiti na uchimbaji wa madini kwenye
Halimashauri hiyo kufanya
shughuli hizo bila kulipoti kwenye
uongozi wa Serikali za vijiji husika na
matokeo yake kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara baina ya makampuni na wanchi
Alifafanua
hata Halishauri yake ya Nsimbo
haifahamu idadi ya makampuni
yanayofanya shughuli kwa kuwa makampuni hayo yanakuja na kuanza
shughuli hata huwa hayatowi taarifa kwenye Halimashauri
Diwani wa Kata ya
Machimboni Raphael Kalinga alieleza kuwa
katika eneo la Mkoa wa Katavi Halimashauri ya Nsimbo ndio kunako patikana madini kuliko maeneo
mengine ya Halimashauri za Mkoa wa Katavi lakini wameshindwa kunufaika na
makampuni ya uchimbaji wa madini
Alisema yapo makampuni yamekuwa yakipewa
leseni za utafiti wa kuchimba
madini lakini badala ya kufanya
shughuli za utafiti wamekuwa wakifanya
shughuli za chimba madini badala ya utafiti
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment