Home »
» Hatari: Watu wanane wamekufa Hapo hapo kwa ajari ya fuso na 11 wajeruhiwa
Hatari: Watu wanane wamekufa Hapo hapo kwa ajari ya fuso na 11 wajeruhiwa
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu nane wamekufa hapo baada ya Roli aina ya FUSO waliokuwa wakisafiri kupinduka na wengine kumi na moja kujeruhiwa na kulazwa hospitalini baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la mlima Katete uliopo katika Kijiji cha Milumba Kata ya Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Ajari hiyo ambayoililihusisha Roli aina ya Fuso lenye namba za usajiri T 234 AXK lilikuwa likiendeshwa na Jamali Mohamed(42) Mkazi wa Mbagala Dares salaam ilitokea hapo Jana majira ya saa kumi na moja asubuhi katika eneo la mlima Katete barabara itokayo Kibaoni W Ilayani Mlele kuelekea Sumbawanga Mkoani Rukwa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi aliwataja waliokufa kuwa ni Peter Lusambo (24),Ngelela Shaulitanga (29), John Pius(32) , Linus (30) aliyetambulika kwa jina moja wote hao wakazi wa Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Kidavashari aliwataja waliokufa wengine kuwa ni Makono Kisumu (23) Elias Mussa(28) wakazi wa wilaya ya Geita Mwanza Ally (34)Mkazi wa Dares salaam ambae alikuwa utingo wa gari hilo na Abasi (28) alitambulika kwa jina moja mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel Wilayani Mpanda
Kamanda Kidavashari aliwataja majeruhi wa ajari hiyo ambao ni Kaswagula Linusi 25 Peter Mkalala 30 Peter Lusambo 20 Castory Kaombwe 23 Nassor Ramadhan 22 wakazi wa Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Wengine ni Salim Hassan 42 mkazi wa Mwanza Jamari Mohamed 42 Salumu Njomoke 22 wakazi wa Dares salaam John Chambaneje 32 Mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hoteli mjini Mpanda
Kamanda Kidavashari alisema chanzo cha ajari hiyo ilitokana na gari hilo kukatika Propela shafuti hari iliyo pelekea gari kuacha njia na kupinduka
Alisema majeruhi hao wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na wanaendelea kupatiwa matibabu na hari zao zinaendelea vizuri
Kidavashari alieleza Dreva wa gari hilo lililopata ajari amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment