Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu Blog
Mtu mmoja mvuvi
maarufu wa samaki aliyefahamika kwa jina
la Credo Amando (KAMANYOLA) 58 Mkazi wa Kijiji cha Majomoto Wilaya ya Mlele Mkoani hapa ameuwawa baada ya kupigwa na kitu kizito
kichwani na mwili wake emekutwa Mvuvi wa samaki
auwawa na watu wasiofahamika
mwili wake wakutwa ukiwa kwenye Ngarawa mtoni
ukiwa kwenye
Ngarawa pembezoni mwa Mto
Kwa mujibu ya taarifa aliyoitowa hapo jana ofisini kweke mbele ya waandishi wa Habari na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo
Agosti 29 mwaka huu majira ya saa saba
mchana
Alisema siku hiyo
ya tukio marehemu aliondoka nyumbani
kwake majira ya saa tatu asubuhi na
kuelekea kwenye shughuli zake za kila
siku za uvuvi wa samaki kwenye mto Kavuu ulipo kwenye Kijiji hicho cha Majimoto
Kidavashari
alifafanua ilipofikia majira ya saa saba
mchana wavuvi wenzake waliokuwa wamefika kwenye eneo hilokwa lengo kuvua samakwaliona Ngarawa pembezoni mwa mtohuku
ndani yake mkiwa na mtu amelala
Alisema wavuvi
hao waliamua kwenda ilipokuwepo Ngarawa
hiyo na ndipo walipoweza
kuuona mwili wa marehemu Credo
ukiwa ndani ya Ngarawa pembezoni mwa mto
Kavuu huku marehemu akiwa na majeraha
makubwa sehemu mbalimbali za mwili wake
Wavuvi hao
walikwenda kutowa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji ambao nao
walitowa taarifa kwenye kituo cha Polisi
cha Maji moto ambao walifika kwenye eneo hilo na kisha mwili wa marehemu
ulifanyiwa uchunguzi wa kidakitari na kubaini
kifo hicho kilitokana na marehemu kupingwa na kitu kizito kwenye sehemu
mbalimbali za mwili wake
Kamanda
Kidavashari alisema katika tukio hili hakuna mtu wala watu walikamatwa
kuhusiana na tukio hili kabla ya kifo hiki
marehemu alikuwa akikorofishana na watu mbalimbali Kijijni hapo kutokana na tabia yake ya
ulevi uliokithiri wa unywaji wa pombe
Jeshi la Polisi
linaendelea na upelelezi wa
kuwasaka wahusika au muhusika wa
tukio hili kuwakamata na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment