Home »
» AUAWA NA MWILI WAKE KUKUTWA KATIKA KISIMA CHA MAJI
AUAWA NA MWILI WAKE KUKUTWA KATIKA KISIMA CHA MAJI
N a Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mary Magese (39) Mkazi wa Kijiji cha Itenka Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amekutwa akiwa ameuwawa na mwili wake kutupiwa kwenye kisima cha maji
Tukio hilo limetokea hapo Septemba 14 mwaka huu majira ya saa mbili usiku kijijini hapo mara baada ya marehemu kumaliza kula chakula cha usiku akiwa na mume wake Razaro Maziku(40)
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema mara wanandoa hao wawili walipomaliza kula chakula mume wa marehemu Razaro Maziku alimuga mkewe kuwa anakwenda nje bafuni kuoga
Alisema Razaro alipomaliza kuoga alirudi chumbani kwake ambako alikuwa amemuacha mkewe na hakuweza kumkuta mkewe hari ambayo ilimfanya amtafute kwenye maeneo ya nyumba yao waliokuwa wakiishi pamoja
Kamanda Kidavashari alifafanua baada ya kumtafuta kwa muda mrefu bila kumuona ndipo mume huyo wa marehemu alipoamua kwenda kumtafuta kwa majirani na kwa ndugu zake lakini hakuwaza kumpata
Siku iliyofuata majira ya saa mbili asubuhi kulizagaa taarifa kuwa kuna maiti imeonekana kwenye kisima cha maji huku ikiwa inaelee kwenye maji ya kisima
Alisemabaada ya taarifa hizo kufika kwenye uongozi wa Kijiji viongozi wa kijiji waliondoka wakiwa wamefuatana na wananchi hadi kwenye eneo hilo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa unaelea juu ya maji na marehemu aliweza kutambulika kuwa mke wa Razaro Maziku
Kidavashari alieleza uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji hayo kimetokana na wivu wa kimapenzi baina ya mume wa marehemu Razaro Maziku na Shija Joseph ambae alikuwa akituhumiwa kuwa hawala yake na marehemu wa muda mrefu hari ambayo ilikuwa ikiwafanya marehemu kuwa na ugomvi wa mara kwa mara na mumewe
Alisema jeshi la polisi linamshikilia mume wa marehemu kuhusiana na kifo hicho kwa mahijiano zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya kuwa upelelezi umekamilika
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment